INASEMEKANA WAWILI WAPIGWA RISASI ZANZIBAR
Watu wawili wanadaiwa kupigwa risasi na mmoja kujeruhiwa vibaya huko
Makunduchi kwenye uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Kheri Makame Hassan (42) na Ramadhan
Hijja Hassan (29) Ali Seif Issa (38). Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Kusini Unguja Juma Saadi amesema hana taarifa za watu kupigwa risasi na
taarifa alonazo ni kwamba risasi imepigwa juu kwa bahati mbaya.
Dk Seif Suleiman wa Hospitali wa Al Rahma amethibitisha kupokea majeruhi na amesema anasubiri picha za X Ray ili kujua majeraha hayo yametokana na nini lakini katika uchunguzi wa awali umeonesha kuwa majeraha hayo huenda ikawa ni risasi kutokana na kuwacha uwazi katika miili yao. Hadi sasa majeruhi hao wamelezwa hospitali ya Al Rahma wakipatiwa matibabu ambapo mmoja hali yake ni mbaya.
Kama tulivyo ipokea kutoka vyanzo mbalimbali