Bukobawadau

KUMEKUCHA MISS KILIMANJARO AMBASSADOR 2015

 Shindano la Miss Kilimanjoro Ambassador 2015 limepamba moto kwa kuchukua sura mpya kwenye vyombo vya habari likiwa na mvuto wa aina yake.
Warembo wanaowania taji hilo wako kambini kwa sasa wakinolewa vilivyo ikiwa ni maandalizi ya fainali za shindano hilo litakalofanyika julai 24 katika ukumbi Kili Home mjini Moshi.
 Habari za kuamianika toka kamati ya maandalizi imesema kuwa kamati imejipanga kisawasawa kuhakikisha wanakidhi kiu ya wapenzi wa tasnia ya urembo katika mikoa ya kaskazini  ikiwemo Arusha ,manyara na Kilimanjaro kwa ujumla.
Pamoja na burudani toka kwa washiriki hao kutakuwa na burudani ya wasanii wa bongo flava,ngoma za asili na saplaizi ambayo haijawahi kutokea katika mkoa wa Kilimanjaro katika anga za burudani.
Kiingilio cha siku hiyo V.I.P(A) ni Tsh 200,000/= ikijumuisha chakula na vinywaji, V/I.P(B) ni Tsh 100,000/= pamoja na vinywaji, SILVER ni Tsh 50,000/= na REGULAR ni 30,000/=
Next Post Previous Post
Bukobawadau