Bukobawadau

LUGOYE WATOA MSAADA WA VIFAA VYA MATIBABU ZAHANATI YA KYELIMA-ISHUNJU

Mwenyekiti wa Lugoye Prof.Joseph Kahamba akimkabidi diwani wa kata ya Ishunju ,Valelia Kato  (kulia) kifaa cha kisasa cha kupima damu ,microscope ya kisasa kupimia magonjwa mbalimbali .
 Vifaa vilivyotolewa  katika Zahanati hiyo ya kijiji cha Ishunju iliyopo kata ya Ishunju, tarafa ya Kiziba ni pamoja na mashine ya kupima shinikizo la damu (BP) na vifaa vya kujizalisha (delivery kits) vyenye thamani ya shilingi milioni moja laki mbili ,Tshs. 1,200,000/=
 Mwenyekiti wa Lugoye Prof.Joseph Kahamba  ambae niDaktari katika Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Hospitali ya Muhimbili (MoI),aki- assemble kifaa kimoja baada ya kingine
Mwenyekiti wa Lugoye Prof.Joseph Kahamba akikabidhi mashine ya kupima shinikizo la damu
Pichani kulia ni Mzee Festo Kahamba,baba mzazi wa Prof.Joseph Kahamba (kushoto)
Bi Magadelena Felisian ,ambaye ni nesi katika zahanati hii akitoa huduma kwa Mzee Felix Bakuza kwa kutumia mashine ya kupima shinikizo la damu (BP),iliyotolewa leo hii na Wanalugoye.
Katika picha ya pamoja kutoka kushoto ni Mwenyekiti  wa Serikali ya Kijiji Kyelima Bw. Vincent Kamugisha,Mh.Diwani Valeria Kato,Mwenyekiti wa Lugoye Prof.Joseph Kahamba,Mganga wa Zahanati Bw. Osward Mwakuku na wa mwisho kulia ni Bwana Edwin Kahamba.
TAZAMA SEHEMU YA VIDEO WAKATI  PROF KAHAMBA AKIKABIDHI VIFAA HIVYO   Huu ni muendelezo wa msaada kutoka kwa umoja wa Wanalugoye wenye masikani yao jijini Dar es Salaam
Next Post Previous Post
Bukobawadau