MANENO YA TUNDU LISSU KUPITIA FACEBOOK
Edward
Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa
UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political
figure in the country right now. Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi
CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake
na Kashfa ya Richmond mwaka 2007. Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo
lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu
kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa
urais. Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea
wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya
kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia
yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande. Kwa
mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na
mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya
kujenga chama tangu 2010. Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo
mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao
kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo
mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana. Kwa kuingia kwake CHADEMA na
UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very
much within our reach. Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana
nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote.
Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui
mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake: Edward Lowassa mtuhumiwa wa
ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha
na kulinda ufisadi. Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa
wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala. Tumemkaribisha Edward
Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo
tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.