Bukobawadau

"MSINGI WA UMOJA NA MSHIKAMANO WA TAASISI YOYOTE NI HAKI" DR.E.NCHIMBI

Dr Emmanuel Nchimbi ambaye ni mbunge wa Songea Mjini kwa tiketi ya CCM, Jumamosi ya leo  July 4,2015 kupitia ukurasa wake wa facebook ameyasem haya:Mwaka huu tunachagua Rais na wabunge. CCM imeanza mchakato wa kupata mgombea wake wa Urais, leo nawarejesha kidogo katika historia. Mwaka 2002 waziri wa mambo ya nje wakati huo mhe Jakaya Mrisho Kikwete alishaonyesha dhamira ya kugombea Urais, na kwa kuwa alikuwa na timu nzuri ya kampeni ilishaanza kuonekana dhahiri kuwa hana mpinzani. Wapinzani wake hawakubaliana na hali hiyo hapo ndipo mikakati mizito ya fitina uongo na uzushi ikaanza kupangwa na kutekelezwa, leo nitaongelea zengwe moja dhidi yake na wafuasi wake. Kikosi cha Uzushi kikaamua kutumia uchaguzi wa CCM Taifa kama kiwanja chao cha mchezo mchafu kikaandaa uongo wa aina mbili kama ifuatavyo

1. Mhe kikwete na timu yake wamepanga kutenganisha kofia ya mwenyekiti wa Chama na Rais ili kumpunguzia nguvu Rais Mkapa.
2. Mhe Kikwete na timu yake wanafanya kampeni nchi nzima kushawishi wajumbe wampigie kura za hapana mwenyekiti wa CCM mhe Rais mkapa.
Dhamira ya wapangaji wa mipango hiyo ilikuwa kwanza kujenga uhasama kati ya Mhe Mkapa na Mhe kikwete pili kufanya wana CCM wamdharau mhe Kikwete na waache kumuamini.
Mbinu hizi kwa kiasi fulani ziliathiri matokeo ya Uchaguzi
Baadae Chama kilibaini kuwa yote hiyo ilikuwa michezo michafu isiyo na ukweli, Mwenyekiti Mkapa alikerwa na jambo hilo na akachukua hatua kuhakikisha kuwa halirudiwi tena.
Nimeandika haya ili kuwakumbusha mabingwa wa fitina na uzushi wa 2015 kuwa hawana jipya michezo wanayofanya wao leo wafitini wenzao waliifanya 2002 kwa maneno na mbinu hizo hizo na tuliokuwepo tupo.
 MSINGI WA UMOJA NA MSHIKAMANO WA TAASISI YOYOTE NI HAKI.
BUKOBAWADAU BOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu ,pia kwa taarifa au shughuli yotote kama kurusha habari na Covarage ya matukio kwa ajili ya kumbukumbu na ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043, 0715 505043 ,0768 397241,0673 505045 Email:bukobawadau@gmail.com Insta:@bukobawadau Insta:@NyumbaniStudio FB page: Bukobawadau Entertainment Media Twitter #bukobawadau
Next Post Previous Post
Bukobawadau