SABASABA WINDHOEK LUNCH PARTY ILIVYOJUMUISHA WADAU WA VIP WAKITAIFA NA KIMATAIFA KATIKA UKUMBI WA DANKEN HOUSE MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited James Rugemalira akitangaza nia na kuwakaribisha wageni mbalimbali katika hafla hiyo ya Sabasaba Windhoek Lunch Party.
Bwana Rugemalira (kulia) akimweleza jambo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kansa kutoka nchini India Profesa. Antony Pais walipokutana katika hafla hiyo.
Bwana James Rugemalira (kulia), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Ukanda Maalumu wa Kiuchumi Mkoa wa Tanga, Chris Incheul Chae ambaye pia hakukosa kuhudhuria hafla hiyo.
Bwana Rugemalira (kulia ) akisalimiana na Mwanyekiti wa Kamati ya Mahusiano na Umma wa Kampuni ya Mabibo Beer wines and Spirits Limited, Anic Kashasha.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Secelela Balisidya naye alikuwepo kuhakikisha mambo yanaenda sawa.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Alice Marco (kulia) naye alikuwepo kuhakikisha kila mgeni anapata vinywaji vya Windhoek vya kutosha. Hakuwa na mzaha katika swala hilo.
Mdau Faustine Kapama (kushoto) na mawakili Paschal Kamala na Sosten Mbedule walikuwepo kufurahia kinywaji murua cha Windhoek.
Ni wageni wengi walikuwepo kuhudhuria hafla hiyo.
Unaona mambo yanavyochangamsha? ni Windhoek tu kwa kwenda mbele.
Huwezi kuamini ilikuwa furaha kila kona.
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Benedicta Rugemalira (kushoto) na mwanasheria wa kampuni hiyo, Respicius Didace (kulia) wakiwa na wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi walipohudhuria hafla hiyo.
Dk. Dee (kulia), akiwa na madaktari wengine katika hafla hiyo.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712727062)