WALIMU SABA TOKA KAGERA WANYAKUA VIKOMBE VITATU NCHINI UJERUMANI CHINI YA SHIRIKA LA JAMBO BUKOBA
Mkoa wa Kagera umeipokea rasmi
timu ya Walimu saba waliokwenda nchini Ujerumani chini ya uratibu wa shirika
lisilokuwa la kiserkali la Jambo Bukoba katika mji wa Berlin kushiriki michezo
na kunyakua vikombe vitatu vya ushindi.
Walimu hao saba kutoka katika
Halmashauri za Wilaya za Biharamulo, Bukoba Manispaa, Misenyi, Karagwe na
Kyerwa, walioratibiwa na shirika la Jambo Bukoba likishirikiana na Serikali ya
Mkoa wa Kagera waliondoka nchini tarehe 27/06/2015 na kuelekea nchini Ujerumani
kushiriki michezo chini ya shirika lijulikanalo kama Discover Footbal na
kurejea nchini tarehe 6/07/2015
Bw. Stephen Gonzaga Meneja wa
Jambo Bukoba ambaye aliongozana na timu hiyo alilielezea shirika la Discover
Football kuwa linajihusisha na michezo kwa akina mama kwa dunia nzima ambapo
huitisha nchi mbalimbali kushiriki kwa pamoja katika michezo ya wanawake hasa
mpira wa miguu.(Kauli mbiu ya shirika hilo ni (Sports without borders and
orders to women).
Bw. Gonzaga alisema Shirika la
Jambo Bukoba lilifanikiwa kupata nafasi ya kushiriki katika michezo hiyo baada
ya kukidhi vigezo kati ya nchi 400 kutoka ulimwenguni zilizoomba nafasi hiyo
Tanzania ni kati ya nchi 100 zilizopata nafasi na kushiriki kwenye michezo hiyo
nchini ujerumani.
Katika bara la Afrika nchi
zilizofanikiwa kupeleka timu katika michezo hiyo pamoja na Tanzania ni Benini,
Bukina Faso, Uganda, Rwanda, Uganda na Afrika ya Kusini. Nchi hizo ziliungana
na nchi nyingine toka katika mabara yote na kuunda timu mbalimbali za ushindani
zilizoshindana na kupata vikombe.
Kaimu Katibu Tawa Mkoa Bw. Eldom
Anyosisye akiipokea timu hiyo alilishukuru shirika la Jambo Bukoba kwa
ushirikiano ambao umekuwepo kati yake na serikali ya mkoa wa Kagera, aidha aliwasistiza
walimu hao walioshiriki michezo hiyo kutoa ujuzi na weledi walioupata katika
wilaya zao hasa katika shule kwa wananfunzi.
Nao walimu walioshiriki katika
michezo na kufanikiwa kupata vikombe vitatu walitoa ushuhuda wa ujuzi wa
kucheza mchezo wa mpira na ujuzi mbalimbali walioupata. Pia walihaidi kutoa
ujuzi huo katika Halmashauri zao hasa kwa kuwafundisha walimu wenzao na
wanafunzi kwa ujumla.