Bukobawadau

JAMES MBATIA AKABIDHI ZAWADI KWA BINGWA WA MASHINDANO YA JIMBO LA VUNJO (MBATIA CUP 2015)

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi,James Mbatia akiwasili katika uwanja wa Himo Polisi kwa ajili ya kushuhudia fainali ya Mashindano ya Kombe la Jimbo ,maarufu kama Mbatia Cup 2015.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi taifa,James Mbatia akisamiana na wachezaji wa timu ya Wazalendo fc kabla ya kuanza kwa mchezo.

Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi,James Mbatia akikagua kikosi cha wachezaji wa timu ya Himo fc.

Kikosi cha timu ya Himo fc.
Kikosi cha timu ya Wazalendo fc.
Heka heka zikiendelea uwanjani.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi,James Mbatia akizungumza wakati wa fainali hiyo kaba ya kukabidhi zawadi kwa mabingwa wa mashindano hayo.
Mmoja wa waratibu wa mashindano ya Kuwania kombe la Mbatia,Danielson Shayo akisoma risala ya mashindano hayo wakati wa fainali hizo.
Mh Mbatia akikabidhi zawadi ya kikombe kwa mabingwa wa mashindano hayo timu ya Himo fc,iliyochomoza na ushindi dhidi ya Wazalendo fc wa bao 2 kwa 0.
Mh Mbatia akikabidhi kitita cha fedha kiasi cha sh Milioni 2 kwa mabingwa hao.
Mh Mbatia akikabidhi zawadi ya mipira mitatu kwa mabingwa hao.
Mh Mbati akikabidhi zawadi ya viatu vya mpira kwa mfungaji bora.
Mh Mbatia akikabidhi vyeti kwa waratibu wa mashindano hayo .
Mh Mbatia akikabidhi zawadi kwa msaidizi wake ,Hamisi Athumani kwa kufanikisha mashindano hayo.
Waratibu wa mashindano ya Mbatia Cup wakiwa katika pcha ya pamoja na Mh Mbatia.
Kikundi cha sarakasi kikionesha umahiri katika kucheza sarakasi katika fainali hizo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.
Next Post Previous Post
Bukobawadau