JARIDA LA EUROMONEY LA UINGEREZA LATOA TUZO YA UFANISI KWA BENKI YA NMB TANZANIA
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto), akiwaonesha waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Tuzo ya Ufanisi wa kibenki nchini Tanzania iliyotolewa na Shirika la Euromoney la Uingereza kwa benki hiyo ijulikanayo Euromoney 2015 Award for Excellence. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa benki hiyo, Joseline Kamuhanda.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa benki hiyo, Joseline Kamuhanda (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
BENKI ya NMB imetajwa kuwa Benki bora Tanzania kwa mwaka 2015, na kujinyakulia tuzo ikiwa ni kwa miaka mitatu mfurulizo.
Tuzo hiyo ilitolewa jijini London nchini Uingereza na Jarida la Euromoney linalojihusisha na masuala ya fedha.
Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ineke Bussemaker alisema Jarida ilo huandaa hafla ya kuyatambua Zaidi ya Makundi 20 ya bidhaa za taasisi za kifedha, ili kutazama benki bora.
Alisema Tuzo hiyo huzitambua pia taasisi za kifedha duniani kote ambazo zimepata mafanikio ya hali ya juu katika shughuli zake, hasa kwa kuonesha ubunifu na kupata mafanikio ya kifedha kila mwaka.
Alifafanua kuwa kazi ya kutafuta washindi, ufanywa na Jopo la wataalam kutoka mataifa mbalimbali na wenye utaalamu mbalimbali, ambao hupitia taarifa zinazowasilishwa na taasisi zote za kifedha duniani na kutangaza washindi.
"Katika miezi 12, benki ya NMB imeanzisha huduma mbali mbali za kibenki na hivyo kuendelea kuwafikia wateja wa huduma za kibenki kuanzia kuweka akiba, kutoa na kuchukua fedha mijini na vijijini"alisema
Bussemaker alitoa shukrani kwa wateja wa Benki hiyo, wafanyakazi na washika dau wote kwa kuwa sehemu ya mafanikio hayo.
Aliongeza kuwa tuzo hiyo inaongeza kwenye hazina ya tuzo ambazo benki imezipata katika miezi 12 huku akizitaja baadhi kuwa ni benki bora ya mwaka kutoka jarida la Banker, Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wakiipa NMB tuzo ya mlipakodi anaefuata sharia katika taasisi za kifedha nchini.