MISS KILIMANJARO AMBASSADOR 2015 YOLANDA SHAYO AINGIZWA MITINI NA MUANDAJI
Muandaji wa
shindano la Miss Kilimanjaro Ambassador 2015,Jackline Chuwa adaiwa kuingia
mitini na fedha za zawadi za warembo na malipo kwa watu aliofanya nao kazi
kufanikisha shindano hilo.
Habari za
uhakika kutoka ndani ya familia ya mshindi wa shindano hilo zinasema kuwa vikao
vya mara kwa mara hufanyika kupanga mkakati wa kuvamia ofisi za BASATA kujua
hatma ya binti yao Yolanda shayo.
ILIKUAJE:
Wakati wa
kutangaza matokeo ya ushindi siku ya fainali za mashindano hayo usiku wa julai
24,mshindi alikabidhiwa Televisheni kama zawadi na kiasi cha pesa kilichoadiwa
kutolewa na mdhamini mkuu ambae ni Coca cola.
Cha
kustaajabisha muandaji huyo alienda ofisi za kampuni hiyo na kuchukua kiasi
hiko cha fedha ikiwa ni zawadi ya mshindi wa kwanza lakini mpaka leo mrembo
huyo anahaha kupata zawadi yake.
Yolanda
aliamua kufunga safari mpaka ofisi za Bonite Bottles na kuwauliza wahusika
kuhusu zawadi yake na alijibiwa kuwa muandaji huyo alishakabidhiwa fedha hizo
siku nyingi.
Jackline Chuwa
Mrembo huyo
alichukua hatua nyingine ya kumpigia simu Jackline na kumuulizia kuhusu zawadi yake
ya fedha taslimu alioadiwa jukwaani na wadhamini wakuu,chakushangaza muandaaji
huyo alitoa kauli ya kumvunja moyo kwa maana hatoipata kabisa kwa kisingizio
eti hakupata faida.
FAMILIA YA YOLANDA:
Familia ya
mrembo huyo imechukizwa na kitendo cha muandaaji huyo kwa kuingia mitini na
zawadi ya binti yao na bila kumkabidhi mikononi mwa kampuni hiyo ambapo ilitoka
ahadi kuwa atakuwa balozi wa kampuni hiyo kufanya kazi mbalimbali kama balozi
wa kinywaji hiko mkoani humo.
Wazazi wa
mrembo huyo wamedhamilia kutinga ofisi za BASATA kufatilia mkataba wa bitni yao
kutokana hali ya sintofahamu kuendela toka binti yao atawazwe kuwa mshindi
mnamo julai 24.
Pia
wanafamilia wametoa shutuma nzito kwa shindano hilo wakihoji ni kwanini msanii wa bongo flava anapewa milioni 25
kutumbuiza wakati binti yao ambae ndiye mshindi anambulia zawadi ya televisheni
pekee.
Yolanda Shayo
WASHIRIKI WENGINE:
Hali ni tata
pia kwa washiriki wa walioingia tano bora hasa namba nne ambae alizawadiwa laki
nne na mapazia kutoka kampuni ya Mapazia house lakini chakushangaza muandaji
huyo aliingia mitini na fedha hizo na kumuacha mrembo akirudi nyumbani na
mapazia tu.
Mrembo huyo
Willice Donard amelalamikia kitendo cha muandaji huyo kumjibu majibu ya dharau
pale alipompigia simu kuulizia zawadi yake.
Habari
zinasema kuwa mrembo alieshika namba tano,Femy Lema alipokonywa nusu ya kiasi
cha fedha alichokabidhiwa jukwaani ikiwa ni zawadi ya kuingia tano bora.
KAMATI YA MAANDALIZI:
Hali si
shwali kwa upande wa kamati,habari za uhakika toka kwa watu walioshiriki kumpa sapoti muandaaji
huyo zikizadai kuwa amewaingiza chaka na kuwazulumu haki yao ya malipo,mpaka
sasa hawajui fedha zao watazipataje.
KAULI ZA MUANDAAJI:
Kauli za
muandaji zilizojaa dharau na kejeli kwa watu wanaodai haki zao ndizo
zilizowapandisha hasira na kufanya baadhi ya watu kutoboa ukweli huu kwani
amekuwa akiwaambia anaenidai aende mahakamani huko ndiko haki ya mtu hupatikana
kwa kisingizio eti amesomea sheria.
KUMBUKUMBU ZAKE:
Kumbukumbu
za muandaaji huyu zinaonesha ni mtu ambae anapenda mambo ya ujanja-ujanja na
kujipatia faida kubwa kupitia majina ya watu kama alivyotaka kumtumia Zari Hassan
kuvuta watu wengi kuingia katika tamasha lake na angali hakuwa na mkataba
wowote na Zari.
Kitendo hiko
kilimfanya Diamond Platnumz kutaka kususia na kuandika maneno makali katika
ukurasa wake wa instagram,kitu kilichompelekea kutozwa faini na uongozi wa Zari.
BASATA:
Wito
umetolewa kwa balaza la sanaa kuwa makini kwa kutoa vibali kwa waandaji wasio
na uhakika na shughuli wanazofanya kama ilivyotokea kwenye hili shindano la
Miss Kilimanjaro Ambassador 2015.
Tunaamini
dhamira ya shindano hili ni nzuri na lina manufaa kwa jamii kuhusiana na utalii,utamaduni
na kazi za kijamii,shindano hili lina faida ila tatizo liko kwa muandaaji
mwenyewe kana kwamba hana malengo na shindano hilo.
Lawama za
pekee ziende kwa Basata kwani shindano hili lilipelekwa kienyeji bila usimamizi
wowote kama ilivyo kwa mashindano mengine makubwa,isitoshe kanuni na taratibu
hazikufuatwa mwanzo mwisho ndiyo maana leo tunapata malalamiko ya mshindi
Yolanda shayo kuingizwa mitini zawadi na mkataba wake.