TUICO YAPATA VIONGOZI WAPYA MKOANI MBEYA
Katibu wa TUICO Mkoa wa Mbeya Ndugu Merboth Kapinga akizungumza na wajumbe wa Tuico siku ya uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Otu jijini Mbeya.(JAMIIMOJABLOG)
|
Wajumbe wa mkutano wakiimba wimbo wa pamoja. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
CHAMA cha
Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri Mkoa wa
Mbeya, kimefanikiwa kupata viongozi wapya watakao kiongoza chama hicho katika
kipindi cha miaka mitano 2015 hadi 2020.
Uchaguzi
umefanyika katika chuo cha wafanyakazi (Otu) jijini Mbeya na kuhudhuriwa na
wajumbe mbalimbali kutoka Taasisi za serikali na binafsi ambao wanawakilisha
chama hicho cha (Tuico) mkoa wa Mbeya.
Akizungumzia
uchaguzi huo, Katibu wa TUICO Ndugu Merboth
Kapinga, amesema uchaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa sheria, kanuni na
taratibu za chama hicho ambacho zinaeleza kuwa kila baada ya miaka mitano ni
lazima chama kichague viongozi wapya.
Amesema,
wafanyakazi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye vituo vyao
vya kazi lakini matatizo hayo yanashindikana kutatuliwa kutokana na mambo
madogomadogo ambayo yanahitaji kupatiwa ufumbuzi kwa pande zote mbili.
Amesema,
wafanyakazi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye vituo vyao
vya kazi lakini matatizo hayo yanashindikana kutatuliwa kutokana na mambo
madogomadogo ambayo yanahitaji kupatiwa ufumbuzi kwa pande zote mbili.
Hata hivyo
amewataka viongozi hao kujenga uwezo wa kupambana na migogoro ya kifedha kwani
ndio changamoto kubwa inayowakabili wafanyaazi na waajiri.
Aidha
amesisitiza kuwa , wafanyakzi ni lazima wawajibike kwanza halafu ndio tudai
haki nzetu kama vile nyongeza ya mshahara na motisha mbalimbali.
Viongozi
hao waliopatikana ni Mwenyekiti wa chama hicho, Willium Mhando pamojana na wajumbe
wa kamati tendaji, Boniface Mwanyamba kutoka kampuni ya vinywaji baridi ya
Pepsi , Joyce Mwakifuna kutoka kampuni ya Coca Cola kwanza.
Wengine ni
Mwanaidi Thadei na Michael Msovakumwao wajumbe kitengo cha biashara,
sekta ya fedha, Winifrida Kinyakisu na Mohamed Tangulia.
Mwisho.