Bukobawadau

VIDEO/PICHA HISTORIA YA MTI AINA YA 'MJUJU' KWA JAMII YA WAHAYA

Katika pitapita zetu za hapa na pale ,Camera ya Bukobawadau Media ikiwa maeneo ya Kibeta inakutana na tukio la Mti huu aina ya 'Mjuju' wenye historia ya aina yake kwa wananchi wakazi wa Mkoa wa Kagera jamii ya (WAHAYA)kwa ujumla ,huu ni  mti unaosadikiwa kuwa na umri yapata karne mbili,Kujua stori kamili  ni kwa nini umekatwa tumeweza kufanya mahojihano na wakazi wa eneo husika kupitia Video iliyopo mwisho wa ukurasa huu....
Muonekano wa Mti huo aina ya Mjuju pichani ,Miti inayopatika maeneo mengi mkoani Kagera na kwingineko ,Nimti wenye historia kubwa katika  matabaka ya Koo zipatazo nane jamii ya wahaya  ambazo ni Bumbira, Edangabo, Ganda-Kyaka, Hamba, Hangiro, Mwani, Nyakisisa, Ekiziba na Yoza (Abayoza)
Historia inaonyesha Katika jamii ya wahaya kuna mambo ambayo ni mwiko au yalikuwa mwiko kuyafanya yaani yamekatazwa kwa mfano kukata mti aina ya Mjuju na Mjunangoma,hii ilikuwa ni kabla ya ujio wa wamissionari
 Mti aina hii ya 'Mjuju na Mjunangoma iliheshimiwa sana kwani hapo ndipo mteni/watemi hutumia kwa ajili ya kufanya matambiko,kwa maana hiyo uchukuliwa/Ilichukuliwa kama mti mtakatifu.
KATIKA VIDEO HAPA CHINI NI MAHOJIANO  NA WAKAZI WA KIBETA KUHUSU MTI HUU
  KUPITIA BUKOBAWADAU MEDIA HAYA NI MACHACHE KUTOKA KWA JAMII YA 'WAHAYA' JAMII ILIYOZINGATIA MAPEMA ELIMU KULIKO MAKABLA MENGINE  NCHINI.
Next Post Previous Post
Bukobawadau