VIP KUSHIRIKIANA NA COSAD CLINIC NA MADAKTARI WALIOPO BUKOBA KUBORESHA HUDUMA ZA UCHUNGUZI NA VIPIMO
Mshauri wa kimataifa
wa kujitegemea wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd Fr. James Rutakwabyera pichani katika akizungumza katika kikao cha washauri wa ndani wa kampuni wa VIP wanaoishi Mjini Bukoba.
Adv Steven Byabato ambaye ni kati ya washauri wa ndani wa kampuniVIP Engineering and Marketing Limited,akitolea jambo ufafanuzi.
1.
VIP ikiongozwa na taarifa za kitafiti kuhusu hali ya ugonjwa
wa Kansa katika Tanzania na hususani ukweli kwamba maeneo ya ukanda wa Ziwa
Victoria yana unyemelezi mkubwa wa magonjwa ya kansa tumejihusisha kufuatilia
ukweli huo na kubaini kwamba pia lipo tatizo kubwa la magonjwa ya saratani
ndani ya Mkoa wa Kagera.
2.
Wakati VIP ikiendelea na mchakato wa kupata ardhi katika eneo
la Kitongo-Makongo ndani ya Manispaa ya Bukoba, kwa ujenzi wa hospitali
kubwa ya kimataifa kwa ajili ya kuchunguza na kutibu maradhiya saratani. tumegundua
kwamba lipo tatizo la kitaalam la kuchunguza na kutambua magonjwa ya aina mbali
mbali. Tatizo hili linaonekana zidi kuwa
kwenye maeneo makuu mawili:
i). Vifaa tiba vya kupima magonjwa
mbali mbali zikiwemo mashine na kemikali (reagents).
ii). Uhaba wa Madaktari na wataalam wa mahabara kuwahudumia wagonjwa.
3.
VIP inatambua na kuthamini kwamba ni watu walio na afya njema
wanaoweza kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za ujenzi wa Taifa. Pamoja na ukweli huo, bado yapo maradhi
ambayo hayahepukiki na mengine yanatokana na jinsi na namna ya maisha yetu ya
kila siku (life style). Lakini pia ni ukweli kwamba mtu akipata maradhi kwa
sababu yeyote ile, basi ili aweze kupatiwa tiba sahihi anapaswa awe amefanyiwa
uchunguzi ulio sahihi ili kugundua tatizo lake.
4.
Ni dhahiri kwamba baadhi ya magonjwa hutokea yakawa sugu na
hata kupelekea kwenye magonjwa hatari ya kansa pale yanapokosekana kutambuliwa
na kupatiwa tiba sahihi kwa wakati ulio sahihi. Kwa hiyo ili kukabiliana na tatizo hilo, VIP inapanga
kuanzisha ushirikiano na COSAD Clinic inayoendesha Zahanati ya kisasa yenye
mashine za kisasa za kufanya uchunguzi wa kimaabara kwa magonjwa mbali mbali,
iliyopo hapa Kashai ndani ya Manispaa ya Bukoba.
5.
Aidha ushirikiano huo utaongezwa nguvu na washirika
wengine muhimu ambao ni madaktari sita ambao wanafanya kazi kwenye hospitali na
taasisi mbali mbali hapa Mkoani Kagera. Madaktari hao wataombwa
kushirikiana na Madaktari wa COSAD, Inc. kutoa huduma kwenye Kliniki ya COSAD
kwa kadiri watakavyojipangia. Ratiba yao
itatangazwa kwa wananchi wote kwa njia
mbali mbali za mawasiliano. Tunakusudia
huduma hii ianze ifikiapo tarehe 15/08/2015.
6.
Ili kuwezesha huduma za vipimo mbali mbali kuweza kuanza kufanyika
kwenye maabara ya COSAD, Inc. VIP Engineering and Marketing Ltd., kwa kuanzia
imetoa msaada wa (reagents) zenye thamani ya TZS. ………….. kwa COSAD, Inc.
kliniki
7.
Kwa wakati muafaka VIP itashirikiana na viongozi wa ngazi
zote katika wa Mkoa na wadau wengine kwenye mpango wa kuhamasisha juu yakupambana
na ugonjwa hatari wa sratania ambao kwa sasa unaongoza kwa kuyachukua maisha ya
watanzania katika rika zote, watoto, vijana, kina mama, wakina baba na wazee hapa
nchinina hata katika nchi jirani.
Adv AaronKabunga Mr. Frank Rutemerwa timu ya washauri wa VIP
Adv AaronKabunga Mr. Frank Rutemerwa timu ya washauri wa VIP
8.
Tatizo la kuongezeka kwa vifo vinavyotokana na saratani limeendelea kuwa ni uelewa mdogo wa jamii juu ya ugonjwa
huo, ambao husababisha wagonjwa wengi kugundulika wakati kansa imekwisha sambaa
sana kwenye mwili na hivyo wagonjwa hao kutokuwa na uwezekano wa kupona.
9.Ni imani ya VIP kwamba kushirikiana kwa dhati katika mpango
huu, tunaweza kutoa mchango mkubwa kunusuru maishaya watu wengi wakati
tukielekea kujenga hospitali kubwa ya kimataifa ya kuchunguza na kutibu
magonjwa ya kansa, Rutakwabyera International Cancer Centre and The Intergrated
Medical Tourism Eco Village.
Mr&Mrs Remidius (Dokta Remmy) wakurugenzi wa Smart Hotel kilipofanyika kikao cha VIP.
Mshauri wa VIP Mwl. Saada Juma pichani katikati akiteta japo na mwakilishi wa VIP Mr. Rahym Kabyemera
Mshauri wa VIP Mwl. Saada Juma pichani katikati akiteta japo na mwakilishi wa VIP Mr. Rahym Kabyemera
Fr. James Rutakwabyera katika picha na Adv .Josephat
Rweyemamu mshauri wa ndani wa VIP.
Imetolewa Bukoba, tarehe 4 Agosti, 2015 na;
Fr. James Rutakwabyera
Mshauri wa kimataifa
wa kujitegemea
VIP Engineering and Marketing Ltd