Bukobawadau

WANACHAMA WA CCM WALIOTEULIWA KUGOMBEA UBUNGE NA UWAKILISHI WA MAJIMBO NA VITI MAALUM KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA 2015



 Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) leo kimetangaza majina ya wagombea ubunge, ubunge viti maalum, uwakilishi na uwakilishi viti maalum ambapo baadhi ya wagombea walioshinda kwenye kura za maoni wametupwa nje na kuchukuliwa mshindi wa tatu.
Akizungumza leo na waandishi wa habari kwenye ofisi za makao makuu ya CCM mjini Dodoma, Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema kuwa kuna baadhi ya majimbo ambayo yamelazimika kurudia kupiga kura za maoni na mengine kuhesabu upya kura zilizopigwa baada ya kujitokeza malalamiko kwa wagombea.

Amesema kuna baadhi ya majimbo ambayo wamelazimika kumchukua mshindi wa tatu kwenye kura za maoni na kuwaacha walioshinda nafasi ya kwanza na ya pili ili kumaliza migogoro iliyokuwepo.

Ameyataja majimbo 11 ambayo yatarudia uchaguzi wa kura za maoni kuwa ni Ukonga, Kiteto, Chilonwa, Kilolo, Njombe Kusini, Makete, Namtumbo, Rufiji, Mbinga Vijijini, Busega na Singida Mashariki.

Aidha Nnauye amesema kuwa uchaguzi wa viti maalum kupitia umoja wa wanawake Tanzania (UWT) yamepitishwa kama yalivyotoka mikoani ambapo ni mkoa mmoja tu wa Dar es Salaam ambao NEC imetengua ushindi wa mshindi wa kwanza, Angela Kiziga ambaye ni mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na badala yake aliyeshika nafasi ya pili na ya tatu ndiyo waliopitishwa katika ubunge wa viti maalum.

Waliopitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM kwenye ubunge wa viti maalum mkoa wa Dar es Salaam ni Mariam Kisangi aliyekuwa mshindi wa pili na Janeth Masaburi aliyekuwa mshindi wa tatu.

WABUNGE WA MIKOA WALIOTEULIWA KUPITIA JUMUIYA YA UWT - ZANZIBAR

NA.
MKOA
JINA
1
Kaskazini Pemba
Ndugu Maida Hamad Abdalla
Ndugu Asya Sharif Omar
2
Kaskazini Unguja
Ndugu Angelina Adam Malembeka
Ndugu Mwanajuma Kassim Makame
3
Kusini Pemba
Ndugu Faida Moh’d Bakar
Ndugu Asha Moh’d Omar
4
Kusini Unguja
Ndugu Asha Mshimba Jecha
Ndugu Mwamtum Dau Haji
5
Magharibi
Ndugu Tauhida Cassian Galos
Ndugu Kaukab Ali Hassan
6
Mjini Unguja
Ndugu Fakharia Shomar Khamis
Ndugu Asha Abdallah Juma


WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI – VITI MAALUM – ZANZIBAR

NA.
MKOA
JINA
1
Kaskazini Pemba
Ndugu Bihindi Hamad Khamis
Ndugu Choum Kombo Khamis
2
Kaskazini Unguja
Ndugu Panya Ali Abdalla
Ndugu Mtumwa Suleiman Makame
3
Kusini Pemba
Ndugu Shadya Moh’d Suleiman
Ndugu Tatu Moh’d Ussi
4
Kusini Unguja
Ndugu Salma Mussa Bilali
Ndugu Wanu Hafidh Ameir
5
Magharibi
Ndugu Mwanaidi Kassim Mussa
Ndugu Amina Iddi Mabrouk
6
Mjini
Ndugu Mgeni Hassan Juma
Ndugu Saada Ramadhan Mwendwa


WABUNGE WA WALIOTEULIWA KUPITIA MAKUNDI MENGINE

NA.
Kundi
WALIOTEULIWA
1.
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)
Ndugu Halima Abdallah Bulembo
Ndugu Zainabu Athuman Katimba
Ndugu Mariamu Dittopile Mzuzuri
Ndugu Maria Ndilla Kangoye
Ndugu Sophia Mfaume Kizigo
Ndugu Irine Uwoya
UVCCM - ZANZIBAR
Ndugu Khadija Nassir Ali
Ndugu Munira Mustafa Khatibu
Ndugu Nadra Juma Mohamed
Ndugu Time Bakar Sharif
2.
Jumuiya ya WAZAZI
Ndugu Najma Murtaza Giga   -    Tanzania Zanzibar)
Ndugu Zainabu Nuhu Mwamwindi  - (Tanzania Bara)
3.
Walemavu
Ndugu Stella Alex Ikupa
Ndugu Amina Saleh Mollel
4.
Vyuo Vikuu
Ndugu Jasmin Tisekwa Bunga
Ndugu Esther Michael Mmasi
5.
NGO’s
Mchungaji Getrude P. Rwakatare
Ndugu Khadija Hassan Aboud
6.
Wafanyakazi
Ndugu Angelina Jasmin Kairuki
Ndugu Hawa Mchafu Chakoma
Next Post Previous Post
Bukobawadau