Bukobawadau

DK MAGUFULI AAHIDI KUKOMESHA MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI NCHINI

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiunganisha alama ya vidole ya V ya Chadema, na kuifanya isomeke W akimaanisha Wananchi atakaowafanyia kazi akiingia Ikulu, baada ya kuchaguliwa na wananchi Oktoba 25, mwaka huu. Alama hiyo aliionesha wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma

Akiwa wilayani Kongwa, Dk Magufuli amesema kuwa akishinda urais atahakikisha anadhibiti mapigano ya kati ya wakulima na wafugaji yanayoendelea nchini na kusababisha vifo vya watu wengi.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG


 Wananchi wakionesha alama ya dole ya CCM ikiwa ni ishara ya kumkubali Dk Magufuli na kuahidi kumpigia kura
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli, akimsimamia Mgombea ubunge Jimbo la Mtera kupitia CCM, Livingstone Lusinde aliyekuwa akifanya mazoezi ya Push Up wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma
 Dk Magufuli akiwapungia mikono wananchi alipowasili kwenye kampeni Uwanja wa Jamhuri Dodoma leo.
 Dk Magufuli akiomba kupigiwa kura na wananchi waliouzuia msafara wake katika Kijiji cha Mbande, wilayani Kongwa alipokuwa akienda kwenye kampeni wilayani Mpwapwa
 Watoto wakiwa wamebebwa ili wapate kumuona vizuri Dk Magufuli katika Kijiji cha Mbande, wilayani Kongwa
 Wananchi wa Kijiji cha Chunyu wakimsikiliza kwa makini Dk Magufuli alipokuwa akitaja vipaumbele vyake atakaposhinda urais
 Mkuu wa Kituo cha Poilisi Mpwapwa Mjini, Mohamed Mhina akiwa kazini wakati wa kampeni za Dk Magufuli wilayani Mpwapwa leo.
 Kijana akiwa na bango lenye maneno ya kumuunga mkono Dk Magufuli wilayani Mpwapwa
 Dk Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Mgombea ubunge Jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Ni furaha iliyoje kwa wasichana hawa baada ya kusikiliza hotuba ya Dk Magufuli katika mkutano wa kampeni Jimbo la Kongwa, Dodoma

Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Kongwa, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai wakati wa mkutano wa kampeni jimboni humo
 Wananchi wa Kibaigwa wilayani Kongwa, wakishangilia kumuunga mkono Dk Magufuli na kuahidi kumpigia kura za ndiyo Oktoba 25, mwaka huu.
 Dk Magufuli akijipigia kampeni  kwa wakazi wa Kibaigwa , wilayani Kongwa leo
 Wakiwa juu ya mti ili wapate kumuona vizuri Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni Kibaigwa, wilayani
 Dk Magufuli akiwaonesha dole gumba wananchi alipokuwa akiwasli kwenye mkutano wa kampeni mjini Dodoma
 Vijimambo vya mkutano wa kampeni za CCM Uwanja wa Jamhuri Dodoma
 Tunda Man akitumbuiza wakati wa mkutano huo
 Mratibu wa Kampeni za Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli (katikati), Abdalah Bulembo (kushoto),  na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa wakijadiliana jambo wakati wa mkutano wa kampeni Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
 Mabango mbalimbali ya kumpigia kampeni Dk Magufuli Uwanja wa Jamhuri DodomaPICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Wasanii wakitumbuiza wakati wa mkutano huo
 Wasanii wa Kundi la TMK Wanaume linaloongozwa na Chege na Tembe wakilishambulia jukwaa wakati wa mkutano huo wa kampeni
 Kundi la wasanii wa muziki wa kizazi kipya la Makomandoo likonesha umahiri wao wakati wa kampeni hizo

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba akiliongoza kundi lake kutumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni za Mgombea urais wa Taznania kupitia CCM, Dk John Magufuli i kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma
 Kundi la TOT likitumbuiza wakati wa mkutano huo
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa  akimuombea kura Dk Magufuli wakati wa mkutano huo
 Dk Magufuli akimshukuru Waziri Mkuu wa zamani, John Malecela kwa kumpigia kampeni katika mkutano huo
 Mawaziri wakuu wa zamani, John Malecela na Joseph Warioba wakipongezana baada ya kumpigia kampeni Dk Magufuli
 Waziri Mkuu wa zamani, Jaji mstaafu Joseph Warioba, akimfanyika kampeni Dk Magufuli ambapo alimfagilia kwa kuhubiri amani katika mkiutano yake ya kampeni kuliko wagombea wa vyama vingine hawasisitizi kudumisha amani nchini jambo ambalo ni tunu ya taiafa
 Dk Magufuli akimshukuru Waziri Mkuu wa zamani, Jaji mstaafu Joseph Warioba kwa kumfanyia kampeni ambapo Warioba alimpongeza Dk Magufuli kwa kitendo chake cha kuhubiri amani katika mikutano yake ya kampeni, tofauti na wanavyokampeni wagombea wenzie bila kutaja  kudumisha amani.
 Dk Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Mgombea ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma leo.
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimvisha kofia aliyekuwa Kampeni Meneja wa Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma mjini kupitia Chadema, katika mkutano wa kampeni za CCM  uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Mfuasi wa CCM akipuliza vuvuzela kunogesha kampeni hizo
Next Post Previous Post
Bukobawadau