Bukobawadau

HABARI PICHA MAPOKEZI YA MWILI WA MZEE JOSEPH MSHUMBUSI MJINI BUKOBA LEO SEP 10.

Mjini Bukoba mamia ya watu na Viongozi mbalimbali wamejitokeza Uwanja wa ndege kushiriki mapokezi ya Mwili wa marehemu mzee Joseph Mshumbusi mapema ya leo majira ya saa 3 asubuhi .
Mara baada ya kuwasili,mwili wa marehemu Mzee Mshumbusi umepelekwa nyumbani kwake maeneo ya Miembeni Uzunguni-Bukoba na kufuatiwa na Ibada maalumu iliyofanyika katika Kanisa Kuu Jimbo katoliki la Bukoba.
 Ibada hiyo imeongozwa na Askofu Mkuu Desiderius Rwoma,kabla ya kuelekea kijijini Kanazi kwa ajili ya shughuli ya mazishi itakayofanyika kesho majira ya saa saba mchana.
  Marehemu Mzee Joseph Mshumbusi ni  Baba ambaye hakuwa na makubwa na aliwapenda watu wote bila kutegemea chochote kutoka kwao, alikuwa mvumilivu na alikuwa mchamungu alilipenda taifa lake na alilipenda Kanisa Katoliki na kulitumikia.
 Inawasili ndege ya shirika la Precission Air ikiwa imebeba kundi kubwa la waomboleza kutoka jijini Dar es Salaam
 Ndege ya maalum iliyobeba  Mwili wa marehemu Mzee Joseph Mshumbusi na wanafamilia ikiwa inatua kwenye wa ndege mjini Bukoba.
 Viongozi wa Dini wakiwa tayari kwa ajili ya mapokezi ya Mwili wa Marehemu Mzee Joseph Mshumbusi.
Wanafamilia wakishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili na mwili wa Marehemu Mjini hapa.
Jinsi walivyo fuatana pichani ni watoto wa Marehemu mzee Joseph Mshumbusi
 Sehemu ya wanafamilia wakishuka kwenye Ndege wakati alipowasili  uwanjani Mjini hapa.
 IGP Mstaafu Said Mwema akishuka kwenye Ndege wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mjini Bukoba
Baadhi ya waombolezaji wakiendelea kushuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili mjini Bukoba.
 Hakika ni za uzuni mkubwa nyuso za wanafamilia, kushoto ni Ndugu Anorld ambaye ni Mtoto Mkubwa wa marehemu, akitoa msaada kwa mama yake mzazi Mjane wa marehemu pichani katikati.
 Vilio vikitawala Uwanjani hapo.
 Sehemu ya wanafamilia mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Mjini Bukoba.
 Baadhi ya waombolezaji waliofika kuupokea Mwili wa Marehemu mzee Joseph Mshumbusi
Stendi maalum iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya kubeba jeneza lenye mwili wa Marehemu mpendwa wetu Mzee Joseph Mshumbusi
 Kijana Sley akiwa tayari uwanja hapo kwa ajili ya mapokezi
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. John Mongella na Mh. Nazir Karamagi
Mzee Karamagi akiteta jambo na Adv.Protas Ishengoma.
 Taswira kutoka nje ya Uwanja wa ndege Mjini Bukoba
 Kushoto ni Haji Abubar Sued, katikati ni IGP Mstaafu Said Mwema
 Ndugu Ludovick pichani kushoto na Ndugu Fabian Kalikawe

Balozi Khamis Kagasheki na Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Jaskon Msome.
Wanafamilia wakikabiliana na majonzi ya mpendwa wao
 Umati wa Waombolezaji nyumbani kwa Marehemu mitaa ya miembeni-Uzunguni Bukoba
 Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Joseph Mshumbusi likiingizwa nyumbani kwake.


Vilio vya hapa na pale kutoka kwa  Ndugu na jamaa wa Marehemu Mzee Joseph Mshumbusi
 Mjini Bukoba hivi ndivyo alivyokuwa amejiandaa Marehemu Mzee Joseph Mshumbusi
 Kabla ya kuelekea kanisani kwa ajili ya Ibada maalum
 Mwanzo wa shughuli ya Ibada iliyofanyika katika katika kuu Cathedral Mjini Bukoba.
 Askofu Mkuu Desiderius Rwoma akiendelea kuongoza Ibada maalum
 Ndani ya Kuu Jimbo katoliki la Bukoba ibada ikiwa inaendelea
 Taswira kanisani Ibada ikiendelea
 Mamia ya Waumini wakiendelea kushiriki Ibada ya mazishi ya MarehemuMarehemu Mzee Joseph Mshumbusi.
 Dada Paschazia Barongo akishiriki Ibada maalum ya kuuombea mwili wa Mzee Joseph Mshumbusi
Shughuli ya Ibada ikiendelea pichani yupo IGP Mstaafu Said Mwema aliye ongozana na mke wake kushiriki mazishi ya rafiki yake Marehemu Mzee Joseph Mshumbusi
 Kushoto anaonekana Ndugu Christoher Chichi
Katikati ni  Kamanda wa Polisi mstaafu, Kamishna Alfred Tibaigana
 Ibada ikiendelea, pichani anaonekana Ndugu Frolence Angelo Mshana
Mratibu wa shughuli ya maziko Ndugu Anic Kashasha pichani kulia
 Adv.Protas Ishengoma akitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia.
 Msafara mkubwa wa magari ukiwasili kijijini Kanazi-Bukoba
 Poleni sana wafiwa wote Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe!!
 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashir Ali akifuatiwa na Ndugu Godwin Barongo na wa mwisho kulia ni Mzee Dauda Mtunzi
Kutoba kushoto ni Bibi Gode,Mrs Chinga na  Dada yake Bi Beatrice.
 Anawasili Msibani hapo kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Agustino Ollomi
Sehemu ya waombolezaji
Hakika ni uzuni mkubwa kwa watu wote.
Ni majonzi makubwa kwa wanafamilia kuondokewa na mpendwa wao, aliyekuwa mpigania Imani mchamungu na mzalendo aliyelipenda taifa 
BUKOBAWADAU BOG tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241
 Ndugu Anic Kashasha mlatibu wa shughuli ya maziko akitolea jambo ufafanuzi
 Muonekano wa kaburi atakapozikwa Marehemu Mzee Joseph Mshumbusi.
  MATUKIO YA PICHA ZAIDI YANAPATIKANA KATIKA UKURASA WETU WA FACEBOOK JIUNGE NASI KUPITIA LINK HII BUKOBAWADAU MEDIA
Next Post Previous Post
Bukobawadau