KAMPUNI YA HUAWEI, BENKI YA NMB, WAMKABIDHI MSAADA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KWA AJILI YA SHULE YA MSINGI KAKUNI ILIYOPO MKOANI KATAVI
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Jimmy Liguo Jin (kushoto), akimkabidhi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda moja ya kompyuta kati ya 50 zilizotolewa na kampuni hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, kwa ajili ya Shule ya Msingi ya Kakuni iliyopo katika Kijiji cha Kibaoni Wilaya ya Mlele mkoani Katavi. Kampuni hiyo imetoa vifaa mbalimbali kwa ajili ya jengo la Tehama kwenye shule hiyo vyenye thamani ya dola za Marekani 150,000. Mradi wa ujenzi wa shule hiyo umefanikishwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kupitia wafadhili mbalimbali.
Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas (kushoto), akimkabidhi , Waziri Mkuu Mizengo Pinda, jezi na mipira vyenye thamani ya sh. 30,000 kwa ajili ya kusaidia shule hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara Serikali wa benki hiyo, Domina Feruz.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia), akitoa maelezo kuhusu mradi huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas, akizungumza kabla ya kumkabidhi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda msaada huo.
.Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Jimmy Liguo Jin (kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda sehemu ya msaada wa Tabuleti 100 zilizotolewa na kampuni hiyo kusaidia wanafunzi wa shule hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni ya HUAWEI nchini Tanzania baada ya kupokea msaada huo.
Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Kikundi cha Ushonaji cha Vijana Sokoine (SYG) kilichopo mkoani Dodoma, Saleh Mustapha akimkabidhi Waziri Mkuu Mizengo Pinda msaada wa Sare za shule aliohutoa kwa ajili ya shule hiyo.
Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Benki ya NMB mara baada ya kupokea jezi na mipira vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 30 vilivyotolewa na Benki hiyo. Kutoka kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano wa Benki ya NMB, Joseline Kamuhanda, Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas, Mkuu wa Kitengo cha Biashara Serikali wa benki hiyo, Domina Feruz na Ofisa Msoko, Jesca Sanga.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto), akiteta jambo na maofisa wa Benki ya NMB, baada ya kupokea msaada huo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara Serikali wa benki hiyo, Domina Feruz na Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta jambo na Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Kikundi cha Ushonaji cha Vijana Sokoine (SYG) kilichopo mkoani Dodoma, Saleh Mustapha.
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amepokea msaada wa vifaa vya shule vyenye thamani ya dola za Marekani 150,000, kwa Shule ya Msingi Kakuni, iliyopo katika Kijiji cha Kibaoni Wilayani Mlele Mkoani Katavi.
Msaada huo wa vifaa umejumuisha Komputa 50, Tablets 100, Kompyuta mpakato 5, Printers2, Scanners2,Projectors 2, Projectors Screen 2, Power System seti moja na Audio System seti moja, Sare za shule 512 na Viatu jozi 1000.
Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhiwa msaada huo ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Pinda alisema wazo la ujenzi wa shule hiyo alilipata baada ya kuona miundombinu haitoshelezi shuleni hapo ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya vyumba vya madarasa na kuonesha shukrani kwa shule hiyo.
"Nilianza kufanya ukarabati lakini nikabaini kuwa eneo la shule hiyo halitoshi kwani wakati nikisoma haikuwa na wanafunzi wengi ambapo sasa inawanafunzi wapatao 800, niliomba eneo kutoka serikali ya kijiji nikapewa ekari 65 na kuwasilisha ombi la usimamizi kwa halmashauri ya wilaya ya Mpanda ili isimamie," alisema.
Alisema ujenzi wa shule hiyo ulikuwa na makisio ya awali sh.bil 1.3 ambapo hadi sasa kiasi kilichoingizwa ni sh. 785,018, ambayo ni sawa na dola 237,834 ambapo April 2013, ubalozi wa China ukiwa wa kwanza kutoa dola za marekani 200,000, ambazo ni sawa na sh.mil 320.
"Kiasi kilichotumika hadi sasa ni sh. mili 745 na kilichobaki ni sh.mil 40 ambazo ni sawa na dola za marekani sh. 150,000 kiasi kilichotumika na kilichobaki dola za marekani 117,495 ambapo Machi mwaka huu tulipokea msaada kutoka ubalozi wa Japani kwa ujenzi wa shule ya awali kwa watoto 200,"alisema.
Alisema hadi sasa bado ujenzi unaendelea na kwamba kuna uhitaji wa kiasi cha sh. 2,180,650 ili kukamilisha ujenzi na kuongeza kuwa majengo ya shule ya mwanzo yatatumika kama kituo cha uendelezaji wa kilimo.
Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Jimmy Liguo Jin alisema kampuni yao inaamini kuwa elimu ndiyo njia sahihi ya mafanikio na kutengeneza njia katika kuleta maendeleo ya nchi hivyo ni jukumu lao kuisaidia jamii ili uendeleza teknolojia kwa njia ya digitali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kikundi cha Vijana Sokoine Dodoma, Saleh Mustapha alisema wametoa msaada wa sare kwa wanafunzi 574 kwa kila mwanafunzi sare 2 ambapo jumla kuu ni 1148 pamoja na viatu.
Ofisa Mkuu wa Fedha wa National Microfinance Bank (NMB), Waziri Barnabas alisema ni sera ya benki hiyo katika kuisaidia jamii kwa kutoa asilimia moja ya ya fauda baada ya kulipa kodi kwa kutoa madawati yenye thamani ya sh.mil 10 na kompyuta 4.
Pinda ametumia nafasi hiyo kuwaomba wadau wengine wapenda maendeleo wa ndani na nje ya nchi kujitokeza kusaidia mradi huo ambao ni mkombozi kwa watoto ambao watapata elimu katika shule hiyo kuanzia ngazi ya shule ya awali hadi shule ya msingi.
Pinda ametumia nafasi hiyo kuwaomba wadau wengine wapenda maendeleo wa ndani na nje ya nchi kujitokeza kusaidia mradi huo ambao ni mkombozi kwa watoto ambao watapata elimu katika shule hiyo kuanzia ngazi ya shule ya awali hadi shule ya msingi.