MAADHIMISHO YA SIKU YA UTALII DUNIANI BUKOBA JUMAMOSI SEP 26 ,2015
KIONGOZI WA MAANDAALIZI: KIROYERA TOURS. ( WADAU WOTE PIA WANAKARIBISHWA ).KAULI MBIU YA MWAKA HUU : “MAMILIONI YA WATALII NI MAMILIONI YA FURSA.”
LENGO
NI NINI?
Umuhimu wa kuadhimisha siku ya utalii
duniani ni kuhamasisha uelewa katika jamii juu ya mchango wa utalii katika
maendeleo ngazi ya familia na mtu binafsi, kitaifa na kimataifa. Hii ikiwa katika
nyanja nyingi ikiwemo kiutamaduni, kisiasa,
kijamii na kiuchumi.
Siku ya utalii duniani huadhimishwa
kila mwaka tarehe 27 Septemba. Serikali ya Tanzania ni mwanachama wa Umoja wa
mataifa na hivyo huadhimisha siku mbali mbali ambazo zinatambuliwa na Umoja wa Mataifa
kama siku ya Mazingira Duniani, Siku ya wafanyakazi duniani na hivyo husherekea siku hii pia. Wadau wa sekta husika
husaidiana na Serikali kuadhimisha siku kama hizi na pia tarehe ya siku ya
maadhimisho yaweza kubadilishwa kidogo kama kuna umuhimu wa kufanya hivyo.
HISTORIA
YA SIKU HII MJINI BUKOBA:Mji wa Bukoba
ulianza kuadhimisha siku ya utalii duniani
mwaka 2002 na kuendelea kufanya hivyo kila mwaka hadi mwaka 2008.
Kulikuwa na chama cha kuendeleza
utalii mkoa wa Kagera maarufu kama Kagera Tourism Development Association (
KATODEA) ambacho kilifanya mchango mkubwa na katika mwaka 2006, Mkoa wa Kagera ulipata fursa adimu ukawa mkoa
ulioadhimisha siku ya Utalii Duniani kitaifa hapa mjini Bukoba. Huo ndio
ulikuwa ufunguo wa kutambuliwa Mkoa wa Kagera katika ramani za utalii nchini
Tanzania. KATODEA imekuwa haiendelei kwa
muda mrefu sasa.
Kuanzia mwaka 2002 utalii ulikua na
kuanza kuleta mabadiliko endelevu mwaka hadi mwaka. Mahoteli kama Walkgard, Kolping, Victorious Pearch, Smart,
Yaasila Top kwa sasa Bukoba Coop na nyingine nyingi zilijengwa. Kiroyera Tours,
Walkgard hotel, Tausi Curio na Hoteli ya Kamachumu Inn walikuwa mstari wa mbele
kutangaza utalii. ‘Tausi curio shop’ ilikua haraka na kuwa na maduka matatu
yenye kazi za mikono ya hali ya juu na ya kuvutia watalii katika mji wa Bukoba. Watalii walianza kutembelea vivutio mbali
mbali vilivyoko Manispaa ya Bukoba, Bukoba vijijini, wilaya ya Muleba na wilaya
ya Misenyi.
Kazi kubwa ilifanywa ya kuainisha
vivutio mbali mbali vilivyomo Mkoani Kagera kwa msaada wa wizara ya mali asili
na utalii. Vivutio pia viliendelezwa kwa kuwekewa barabara za kupitia watalii,
kutengeneza ratiba za matembezi zinazounganisha vivutio hivyo na kuvitangaza
katika maonesho mbali mbali kama saba saba hapa Bukoba na maonesho ya utalii
kitaifa (huko Arusha na Dar es Salaam) pia maonesho ya kimataifa (Spain,
Uingereza, Milani, Belgium, Ufaransa na Marekani). Vijitabu vya vuvutio hivi
viliandikwa pia na kusambazwa. Katika vivutio hivi kuna mvuto wa Ziwa Victoria
kwenda kisiwa cha Musira, kisiwa cha
hifadhi ya Rubondo (Rubondo Island National Park) na vinginevyo. Kuna msitu wa
Kyamunene na maporomoko ya maji na pango
karibu na Bukoba na maporomoko yam to Bugonzi huko Kamachumu; Wahunzi wa vyuma
wa Itahwa na utaalamu wa asili wa vyuma wa Maruku Zamadamu Katuruka; Mapango ya
michoro ya kale ya Bwanjai –Mugana; chakula na mapishi ya asili, ngoma na
nyimbo za kitamaduni Gera, maarufu kama” kwa mama Kisha” na nyumba za asili za “majani full suit”
maarufu kama “Mushonge museum” huko Kanoni
Kamachumu. Kwa juhudi hizi Kisiwa cha Rubondo ambacho hapo awali
kilikuwa kinapata wageni kwa nadra sana, kwa sasa huwa kinafikia kukataa
kupokea wageni ili kulinda kisizidi viwango na kuathiri uhifadhi wa wanyama na
mazingira.
UKUAJI
WA UTALII MJINI BUKOBA
Ni vyema kusema Bukoba inapokea
watalii halisi kutoka nje 2000 kwa mwaka, ambao wanafika Bukoba kwa ajili ya utalii tu. Kati ya hawa
kuna wanaotaka kuona na kutembelea vivutio vilivyopo hapa Bukoba, na baadhi yao
ni wapita njia, wengine wanatafuta usafiri, wengine wanatafuta huduma ya malazi
na baadhi wanataka kuishi kwa muda katika jamii ya Bukoba na kufanya kazi za
kujitolea. Ni mara nyingi sana kuona magari yakusafirisha watalii kutoka Uganda na Rwanda yakiwa Bukoba.
Ukweli ni kuwa nchi ya Uganda hupata watalii wengi kuliko nchi ya Tanzania.
Baadhi ya watalii kutoka Uganda hupitia mjini Bukoba wakiwa wanaelekea kwenue
mbuga za wanyama za Serengeti na Ngorongoro. Huduma ya usafiri ni muhimili kwa
utalii. Wasafirishaji ni pamoja na kampuni ya ndege ya Auric, Precision Air, huduma za usafiri wa majini MV Victoria na
sasa MV Serengeti ambayo kwa sasa ni
chaguo la watalii wengi wa Bukoba. Pia kuna usafiri wa njia ya barabara Taxi
pamoja na mabasi na boda boda.
AJIRA
KATIKA UTALII
Kwa makadirio ya kuwa watalii 15
hutengeneza ajira ya mtu mmoja, Tuseme angalau wakazi 100 wa Bukoba wana ajira
ya moja kwa moja kwenye utalii kama mahotelini na katika kampuni za utalii.
Tukikadiria kwa wastani muajiriwa mmoja
anawategemezi watano, ni dhahiri kuwa takribani watu 500 hapa Bukoba
wanategemea utalii katika maisha yao.
Biashara ya Utalii inategemea sana
Nyanja nyingi za ugavi (Supply chain) kwa mfano wauza vyakula wa soko kuu, maduka
yanayouza bidhaa mbali mabali kama taa, dawa za miswaki, sukari na vifaa vya
ujenzi. Watoa huduma ya burudani pia wanahitajika kama ajira. Wakulima wa
mbogamboga, matunda, na maua na wafugaji wa kuku na ng’ombe. Pia wauzaji wa
mavazi, mashuka na vitambaa vya meza za chakula, glasi, sahani, uma, visu
pamoja na vijiko n.k. huduma za vinywaji
baridi na vikali, wauza vinyago, wachapishaji wa vipeperushi na internet café,
makampuni ya ulinzi, na wanausalama wote, hawa wote ni wadau wa utalii na wanapatikana
hapa Bukoba.
Tukiunganisha waajiriwa katika Utalii
na wale wanaonufaiuka na utalii kupitia ugavi, tunasema wako watu takribani 1000
wanaopata ajira kutokana na sekta ya
utalii.
JE
NI KWA JINSI GANI MAADHIMISHO YATAFANYIKA MJINI BUKOBA?
TAREHE: Siku ya maadhimisho itakuwa Jumamosi
26 Septemba 2015
MAHALI: Ni katika viwanja vya Kiroyera Tours
vilivyoko katika fukwe za ziwa Victoria, barabara ya Forodhani – Shore Road Kata Bakoba
SHUGHULI:
1. KONGAMANO (ROUND TABLE): Kutakuwepo
na kongamano litakalochukua masaa 2 (mawili) na litaendana na Kauli mbiu ya
mwaka huu inayosema “Mamilioni ya watalii ni Mamilioni ya fursa”.Maongezi
yataendana na maana nzima ya utalii endelevu; Utalii unaolenga kuondoa umasikini, Ukuzaji wa ujasiliamali na
uwekezaji; teknolojia na ufundi na Huduma bora kwa watalii ( Excellence in
Customer care). Wazungumzaji watatokana na wadau. Maswali na majibu yatakuwepo.
2.
MAONESHO: Kutakuwepo
na maonesho mbalimbali ya bidhaa zinazotengenezwa na kuzalishwa na wadau wa
utalii kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Kagera. Bidhaa hizo ni pamoja na za
hoteli za kitalii, vivutio vya watalii, wafanyabiashara wa utalii Tanzania, wasafirishaji
na watoa huduma ugavi kama TANICA, wauza
vinywaji na kazi za mikono wanakaribishwa. Wadau wa utalii wote wote
watakaribishwa kufanya maonesho yao siku hiyo na kwa wanaohitaji meza ya
maonesho italipiwa elfu 20 tu.
3.
MAANDAMANO YA MAGARI NA PIKIPIKI:
Tutawakaribisha wapanda pikipiki 30 na magari kuzunguka mitaa ya manispaa ya
Bukoba kuonesha umuhimu wa sherehe ya utalii
Duniani na watu wote watakaribishwa kushiriki sherehe hiyo.
4.
KUTOA ZAWADI: Aina tatu za huduma ya utalii
zitatambuliwa na kutunukiwa vyeti maalum.
sekta zitakazotambuliwa ni: Hoteli tatu, kampuni
za usafirishaji tatu na vivutio vya watalii vitatu.
5.
KUZINDUA JIWE LA KUMBUKUMBU YA MJERUMANI EMIN PASHA NA KUANZA KWA MJI WA BUKOBA
MWAKA 1890
6.NYAMA
CHOMA: Nyama choma
pamoja na muziki na kucheza ngoma vitakuwapo.
Media: Watakaribishwa waandishi habari na
wapiga picha za video na bloggers.
SERIKALI: Kutakuwepo na viongozi wa serikali
akiwamo mgeni rasmi na TANAPA, Uwakilishi wa wizara husika, Tanzania Tourist Board (TTB) nk. Viongozi hawa
watashiriki katika maadhimosho haya kwa
ufunguzi rasmi, ushiriki katika kongamano, Ushiriki katika maonesho, maandamano
na shamra shamra ikiwemo hotuba rasmi kwa wananchi wote.
NATANGULIZA SHUKRANI.
Imetayarishwa na MARY CONSO KALIKAWE
, Mkurugenzi Mwendeshai KIROYERA TOURS.
Kwa mawasiliano: +255 713526649 au
barua pepe: mkalikawe@gmail.com
MPANGO WA MAONESHO SIKU YA UTALII DUNIANI 26 SEPTEMBER 2015
VIWANJA VYA KIROYERA TOURS BUKOBA
Kutakuwa na Mahema matano 5 yatakayokuwa
yametazama ziwani kwenye sehemu ya uwazi iliyoko kati ya Ofisi za Kiroyera
Tours na upande wa Bar.
2.
Ndani ya kila hema kutakuwa na meza nne ambazo
kutakuwa na kampuni, watu binafsi au taasisi
3.
Jumla ya watakaokuwa wanaonesha ni takribani
unit 25 ambazo ni zifuatazo
i)
Rubondo Island National Park TANAPA
ii)
Tanzania Tourist Board (Mwanza Regional Office)
iii)
Department of Tourism (MNRT DSM)
iv)
SAA NANE Island National Park
v)
Regional Office (RAS Kagera)
vi)
BMC (Bukoba)
vii)
Kyamunene water falls and Cave (Rubale Forest
Bukoba)
viii) Kolping
Hotel
ix)
KAPOTIVE singers
x)
Kagera Museum
xi)
Mama Kisha cultural Gera
xii)
Mushonge Museum Kamachumu
xiii) Thereza
Ntezibwa Women Crafts
xiv) Humpton’s
Café (Bukoba)
xv)
WalkGard Hotel
xvi) Karume
Day Primary School
xvii)
CRDB Bank
xviii)
Kiroyera Tours
xix)
Victorious Perch Hotel
xx)
Zamadamu - Katuruka Iron Technology and cave of
the dead
xxi)
Itahwa Wahunzi wa Vyuma
xxii)
ELCT Hotel
xxiii)
Auric Air
xxiv)
TANICA
Kila mshiriki
anategemewa kulipia ushiriki wa naonesho angalau elfu 20. Wale wakubwa
tumewawekea elfu 50 au laki moja kama gharama ya kushiriki. Hii itachangia
kidogo katika gharama za sherehe hii.
JE KIROYERA TOURS NI
NANI?
Kiroyera
Tours ni kampuni iliyosajiliwa BRELLA mwaka 2001 kwa Reg No… . Ina leseni ya
kuongoza watalii TALA…. Kampuni hii ndio
ya kwanza kuanzisha utalii mkoani Kagera
ikiwa imeanzishwa na wanawake watano wazawa wa mkoani humu. Makao makuu yake ni
hapa mjini Bukoba hata ingawa imefungua tawi huko Dar es Salaam. Kiongozi wa
wanawake hao ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo anaitwa Bibi Mary
Kalikawe. Bibi Mary Kalikawe ni mtaalamu wa mambo ya utalii na alikwisha ajiriwa
na Serikali ya Botswana kwa miaka mingi kama Expatriate mtanzania kabla
hajarudi Bukoba kufungua kazi za kampuni hii. Pia mama huyu ameshafundisha chuo
kikuu cha Dar es Salaam. Maneja wa sasa
wa Kiroyera Tours ni Aaron Kalikawe. Kampuni ina wafanyakazi 15. Kati yao ni
Bw. Superius Kalemera ambaye ni muongoza watalii mzoefu wa miaka mingi, Bi
Methodia Method Maneja wa Kagera Museum na wengineo. Tafadhali tembelea tovuti
ya Kampuni www.kiroyeratours.com na
brochure yetu kwa ufahamu zaidi.
1.0 VIVUTIO VYA UTALII
Mama Mary akiwa anaongoza kampuni
hii ameweza kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa Tanzania Tourist Board TTB na kampuni
imeweza kupata tuzo mbali mbali za kimataifa na kitaifa ikiwemo ya Spain
Millenium Tourism Award, UN Habitat Nairobi,
Ford Foundation, World Bank iliyotolewa nchini Ghana na nyingine nyingi.
Juhudi za Kiroyera Tours zilifanya mkoa wa Kagera uwe na chama bora cha Utalii
kikiitwa Kagera Tourism Association. Kiroyera Tours licha ya kuanzisha kampuni
ya kwanza ya utalii ambayo imedumu kwa miaka 14 sasa hapa mjini Bukoba,
ilifungua Kagera Museum iliyoko Nyamkazi na camping site iliyoko ufukweni shore
Road. Imevumbua na kuendeleza vivutio mbali mbali vya Utalii hapa Mjini Bukoba
ikiwemo kisiwa cha Musila, Maporomoko ya msitu wa Rubale Kyamunene, Maandishi
ya kale ya Bwanjai, Kamachumu, Gera, ulimaji wa kahawa na vanilla kwa watalii
nk. Kwa kazi hizi Bibi Mary Kalikawe aliwahi kuteuliwa akawa Mkurugenzi wa bodi
ya Utalii TTB. Juhudi za Kiroyera zimetangazwa kwenye vitabu vya kimataifa vya
kuongoza watalii kama Lonely Planet, Brandts Guide, magazeti mbali mbali na vyombo kadhaa vya
habari. Kiroyera imepokea na kutembeza watalii kutoka nje ya nchi takribani
elfu Tatu tangu kuanza kwake. Kampuni inazidi kuvumbua na kuunda vivutio zaidi.
2.0 DIRA YA KAMPUNI (Imeandikwa
kwa kiingereza)
2.1 Mission
The Mission of Kiroyera Tours and Consulting
is to widely promote Lake Victoria Zone in particular Kagera Region as a
tourist destination and to operate quality assured tourism services within the
Lake regions and around Dar es Salaam and beyond. Through our consultancy
services, to contribute to capacity building and ensuring Kagera and other
areas of Tanzania make the most of their Natural assets now and for the
future.
2.2 Vision
To sustain Kiroyera Tours and consulting as
a leader in Tourism Development in the East Africa region by maintaining a high
rank among the best companies and a preferred choice for tourists and other
clients.
Tafadhali angalia kijitabu cha
“COMPANY PROFILE” Kiroyera Tours kwa maelezo zaidi.
3.0 USHIRIKISHAJI WA WANANCHI KATIKA UTALII
Kampuni ya kiroyera imefanya
bidii sana kuhusisha wananchi katika faida zinazoletwa na utalii. Tangu kuanza
kwake Kiroyera
3.1 Ajira: imeajiri wafanya
kazi wazawa peke yake hata ingawa imebahatiwa kuwa na Volunteers wengi kutoka
nchi mbali mbali. Hawa wameleta na kubadilishana ujuzi na wafanyakazi
waliowakuta. Wafanyakazi wote wamejifunza kuendesha huduma za utalii wakiwa
wameajiriwa ndani ya kampuni. Tangu kuaza kwake Kiroyera tours imekwisha ajiri
wafanyakazi zaidi ya 50 wengine wamehama na kutafuta kazi mahali pengine. (Kuna
waliajiriwa na kampuni kuubwa kabisa za utalii kutoka Ulaya na Marekani kama
Grumeti (Justin Mwabuki), Asilia (Hamza), wengine wamepata kazi serikalini
(Mariana na Zaharani) na wengine wameanzisha kampuni zao wenyewe za utalii
akiwemo Bi Mariana wa Mama’s Travel Agency ya Mwanza yenye tawi Bukoba na Bw
William Rutta aliyekuwa Maneja wa Kiroyera ambaye ameanzisha kampuni ya Bukoba
Cultural travel.
3.2 Kukodi vifaa vya kazi kutoka kwa wanachi: Baiskeli za
kuzungusha watalii mjini Bukoba na mitumbwi ya kuzungusha watalii ziwani huwa zinakodiwa wananchi wenyewe. Mara kwa
mara tunakodi magari ya kutembeza watalii kutoka kwa wakazi wa mjini Bukoba.
Usafiri wa ndege, meli, mabasi, daladala, pikipiki pia. Hoteli mbali mbali,
migahawa na guest house ni wadau wetu tunapolaza watalii na kupata chakula cha
watalii. Vivutio vya utalii tunatumia vilivyopo katika sehemu za wananchi na
tunakwenda hadi mabali Kamachumu, Mugana, Gera, Missenye nk. kupeleka watalii
na kulipa watu wenye vivutio vyao huko.
3.3 Sokoni, madukani, vifaa vya ujenzi, mafundi, simu na mawasiliano
pia wataalamu (Accountants): Fedha ambazo zimepitia Kiroyera zikaingia sehemu
hizi mbali mbali zinazidi wastani wa milioni 12 kwa mwaka
3.4 Kodi kwa Serikali na michango katika jamii: Kiroyera Tours ni
kampuni pekee inayolipa USD 2000 kila mwaka kwa leseni halali ya kuongoza
watalii na kutimiza masharti yote yanayotakiwa na serikali kupewa leseni hii.
Tunalipa TRA vema kabisa na hata NSSF na ushuru mbalimbali wa Manispaa. Jamii
imeichagua Kiroyera Tours kuwa mahali pa kuzungukia wakiwa wanachagisha
michango ya kila aina!
4.0 WATOTO YATIMA NA WALEMAVU
Kampuni ya
Kiroyera imejihusisha na kuanzisha NGO’s za kusaidia walemavu kama BUDAP (www.budap.org) na Heritage Initiative Bukoba
ambayo imechangia sana kutunza watoto yatima. NGO’s hizi zinajulikana kitaifa
na kimataifa. Uwezo kusaidia jamii kutumia
NGO’s hizi umetokana na watalii wanaopitia kampuni yetu.