MASWALA HAYA NI MUHIMU KATIKA MAHUSIANO
Kinachokupa kiu ya kurudi nyumbani mapema au ya kuwepo nyumbani nyakati ambazo haulazimiki kutoka hakitakiwi kuwa ni Tv programs, au ujenzi unaoendelea nyumbani, au uzuri wa nyumba na sebule yako, au kazi unazotaka kufanya ukiwa nyumbani au nafasi ya kupumzika au kulinda vitu visiende kombo, la hasha, kiu yako inatakiwa kuchochewa na wale uliowaacha nyumbani, kiu ya kuwaona, kukaa nao, kufurahi nao na kushiriki mioyo pamoja nao. This is what makes a HOME differ from a HOUSE-
KUWA MAKINI SANA ISIJE IKALA KWAKO MAZIMA
Yamkini ulidanganyika na muonekano wake wakati anakuja kukuchumbia, ukaangalia sura, aina ya marafiki, story na maneno mengi anayoongea ukadhani huo ndio uhalisi wake na moyoni ukajipa raha kabisa kwamba nimepata mume hapa. Sasa leo umeshaolewa maumivu hayakuishi, jamaa mvivu, hajitumi, anakaa tu wewe ndio utafute na kutunza familia, sasa ndio unagundua hata lile gari halikuwa lake, amekuwa tegemezi kwako ktk kila kitu, moyoni unaona yamekufika kooni lakini huna hata chembe ya confo la kuwaambia wengine maana mwanzoni ulijiona umepata mchongo kumbe mchongoma. Pole mama. Wenzako wakinunua kiatu hawatazami kamba zake bali soli yake - Chris Mauki
INABOA HATA KAMA UNAONA AIBU KUMWAMBIA
Unakuta mumeo yuko very close na mama yake mzazi (hiki sio kitu kibaya ni chema kabisa) sasa chakushangaza mama anamcontrol kwenye kila kitu, hata mkipanga kitu cha kifamilia mama akiingiza ajenda yake hapo kile chakwenu kinakufa ghafla, mama anaweza kumwita mwanae wakati wowote na kokote, mkipanga kitu wewe na yeye basi atamuuliza mama yake kwanza, nyumba yenu mama ndiyo alipendekeza ijengweje na muwekeje vitu. Mbaya zaidi wapo hadi wanaoambiwa na mama vyakula gani kijana wake hupendelea. Mimi najiuliza, kama huyu kijana bado mtamu hivi kwa wazazi sasa walimruhusu vipi akaoe?? Yani sasa binti wawatu kaolewa na wengi. Yataka moyo aisee -Chris Mauki