Bukobawadau

MLANGIRA JUSTUCE LUGAIBULA MGENI RASMI KATIKA TAMASHA LA KWAYA LILILOANDALIWA NA KWAYA YA MT.JOHN BOSCO-BUKOBA CATHEDRAL

Mlangira Justuce Muganyizi Lugaibura pichani ameweza kuhudhuria kama Mgeni rasmi katika tamasha ya kuadhimisha miaka 33 ya Kwaya ya Mt. John Bosco ya Cathedral Bukoba.
 Hivi ndivyo Mgeni Rasmi Mlangira Justuce Lugaibula alivyoingia Ukumbini , huku akisindikizwa na shangwe za nyimbo za mapambio na kumsifu bwana
 Umati wa watu waliohudhuria katika tamasha hilo wakishangilia wakati Mgeni rasmi anaingia katika Ukumbi wa Linas  kushiriki tamasha hilo la kihistoria lililoweza kufana sana.
Mgeni rasmi katika tamasha la kwaya lililoandaliwa na Kwaya ya Mt. John Bostco ya Bukoba Cathedrala ,Mlangira Justuce Lugaibula pichani  na Mke wake Omwana Joilyn Jojo (Jojo) wakiwa katika tamasha hilo lililofanyika jioni ya jana Jumapili Aug 30 ,katika Ukumbi wa Linas na kushirikisha waimbaji wengi wa Manispaa Bukoba na maeneo ya jirani.
Katika tamasha hilo Mgeni rasmi Mlangira Justuce Lugaibula kaongozana na mama yake Mzazi  Bi Grace (pichani kulia) ,pamoja na mambo mengine kwa kutambua mchango mkubwa wa mama yake Mzazi  katika ngazi ya familia na jamii nzima ,Mlangira Justuce amechangia kwaya ya Mtakatifu John Bosco jumla ya shilingi milioni ishirini ( 20m/-).
 Waimbaji wa kwaya ya Mt. John Bosco wakitumbuiza katika  tamasha hilo
Claudi Mutabuzi akiwaongoza wanakwaya wa Mt. John Bosco katika tamasha hilo.
Kkundi cha 'Utoto  Mtakatifu' wakitoa burudani katika tamasha hilo.
 Muimbaji mahiri wa nyimbo za Injili, Mwalimu Mgango akiwajibika jukwaani
 Mwalimu Mugango akiongoza waimbaji wa Kwaya ya BCC.
 Jamaa wa familia walio hongozana na Mgeni rasmi.
 Muonekano wa meza kuu, pichani kushoto ni Fr. Faustin Kamugisha
Sehemu ya wadau waliohudhuria tamasha hili lililoandaliwa na kwaya ya Mt. Bosco Bukoba
 Mmoja wa waimbaji wa Kwaya ya Mt. John Bosco akipiga makofi kwa furaha .
Wadau pichani katikati ni Ndugu Kagunguna akifuatiwa na Ndugu Juvenary wakiwa wameketi wakati tamasha hilo linaenelea
Kikucha cha Ngoma cha Mt. Cecilia kutoka Mutukula border kikishusha burudani.
Burudani ya Ngoma na kuimba  nyimbo za Kiganda ikiendelea .
Fr. Faustin  Kamugisha pichani kulia ,akiagana na Mgeni rasmi Mlangira Justuce Lugaibula
Mlangira Justuce Lugaibula akipokea risala toka kwa katibu wa kwaya ya Mt. John Bosco Ndugu Ndibalema.
 Mc Hima Mgija akifuatilia kinachojiri ukumbini.
Ndugu Rutakwa ambaye ndiye Mc Muongozaji wa shughuli hii akitolea jambo ufafanuzi.
Wananchi waliohudhuria tamasha hilo wakitoa michango yao katika kusopport kwaya ya Mt. John Bosco.
 Ndugu Kagunguna akitoa mchango wake.
 Wanaingia  Jukwaani wanakwaya wa Vijana-Bukoba
Wanakwaya waVijana wakitoa burudani
 Mwenyekiti wa Kwaya ya Mt. John Bosco akitoa neno.
 Mzee pichani akaonyesha kuguswa na maandalizi mazuri na mpangilia wa shughuli hii,nae kama mhudhuriaji akachangia kiasi cha shilingi laki moja (100,000/-) 
 Sehemu ya wadau walioweza kuhudhuria tamasha hilo na kuchangia
Wengine walioweza kuchangia ni pamoja na Ndugu Muganyizi alitoa kiasi cha shilingi Milion moja.
Mzee Kimasha na Mr. Willy wakifuatilia kinachojiri katika tamasha hilo lililoweza kufana sana
Wanakwaya wa BCC katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi.
 Bi Grace  mama mzazi wa Mlangira Justuce akipokea mkono wa pongezi kutoka kwa mwanakwaya
 Pongezi kwa Dada wa Mgeni rasmi pamoja na Mama mzazi
PITIA SEHEMU YA VIDEO INAYOFUATA HAPA CHINI
Next Post Previous Post
Bukobawadau