NAWASHANGAA MAWAZIRI WAKUU WENZANGU WALIOSTAAFU,WAKIDAI CCM MIAKA 50 HAKUNA KILICHOFANYA-JAJI WARIOBA
Waziri
Mkuu Mstafu Jaji Joseph Sinde Warioba akihutubia wakazi wa Butiama
ambapo aliwaeleza Magufuli anafaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MARA
WAZIRI Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, ameibuka katika
kampeni za mgombea urais wa CCM Dk. John Magufuli na kusema kuwa
anashangazwa na hatua ya mawaziri wakuu wenzake kuhama CCM na kudai
hakuna kilichofanyika katika miaka 54 ya Uhuru.
Pamoja na hali hiyo amesema anajua wazi huenda hata
wanachokifanya hawajui wajibu wao walipokuwa katika madaraka hayo kama
washauri wakuu wa rais.alisema sasa umefika wakati wa watu
wanaomtumia kama dira Baba wa Taifa katika kampeni zao wajitafakari
zaidi.
"Wengine katika kampeni zao wanatumia maneno ya Mwalimu
kama wamechanganyikiwa. Huwezi kumtumia Mwalimu kama dira halafu unasema
CCM haijafanya kitu, aliijenga Tanzania kwenye misingi na wote
walimfuata wanapita kwenye misingi yake," alisema Jaji Warioba
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama
cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya wananchi
waliojitokeza katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika mjini Bunda
leo.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akipokea kifimbo na Chief Japhet Wanzagi kwa niaba ya Wazee wa Butiama.
Dkt akionesha fimbo hiyo aliyokabidhiwa na Chief wa Wazanaki,Japhet Wanzagi
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama
cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge kulia ni
Nimrod Mkono kutoka jimbo la Butiama Vijijini na Profesa Sospeter
Muhongo ambaye anatoka jimbo la Musoma vijijini.
Mamia ya Wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe
Magufuli.
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Nyamuswa ambako ndiko alikozaliwa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mgombea Ubunge wa jimbo la Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe. Stephen Wasira,shoto ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba,kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika mjini Nyamuswa jioni ya leo.
Wananchi wa Nyamuswa wakimsikiliza Dkt Magufuli.
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Nyamuswa ambako ndiko alikozaliwa
Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba,wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano.
Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na mgombea
ubunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Ndugu Sospeter Muhongo,kushoto ni Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe. Stephen Wasira wakati wa mapokezi mkoani Mara,pichani kati ni Mtoto wa Baba wa Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Afrika Mashariki,Mh Makongoro Nyerere
Umati wa wakazi wa Butiama wakimsikiliza Mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Sehemu ya Wananchi wa Butiama wakishangilia jambo