Bukobawadau

SIKUKUU YA MTAKATIFU MIKAILI NA WATOTO USHARIKA KIGARAMA K.K.K.T

Picha:Kanisa la Usharika Kigarama K.K.K.T
 Maandamano ya watoto
Mchungaji Diocles Mashongole wakati wa mahubiri
KANISA la K.K.K.T,Usharika wa Kigarama,Dayososi  ya Kaskazini Magharibi linahitaji zaidi ya sh milioni mbili na elfu arobaini kuwa na jingo mahsusi kwa ajili ya Shule ya Jumapili ya watoto(Sunday school).

Hayo yamesemwa na mchungaji wa kanisa hilo,Diocles Mashongole wakati wa Ibada ya Jumapili 27.09.2015 katika kuadhimisha ‘Sikukuu ya Mtakatifu Mikaili na watoto’usharikani hapo.
 Mch.Mashongole(kulia)akiwa na watoto wakati wa mnada wa mazao yao ya shambani
Amewahimiza wazazi kuwa na upendo kwa watoto wao,kuwaelekeza na kuwasaidia ili wawe watu wa kutumainiwa na wazazi wenyewe na taifa kwa jumla,huku akiwahimiza  katika matumizi mzazuri ya mitandao ya kompyuta na runinga kwa kuangalia mambo yanayowafaa,hasa yahusuyo masomo yao.
Aidha mchungaji huyo amewataka wote waliojiandikisha kupiga kura uchaguzi mkuu 25 0ktoba,kuitumia vizuri fursa hiyo kwa kutimiza wajibu huo,huku wakizingatia utaratibu wa kupiga kura ,bila kuwa na viashiria vya vyama vyao kama ,mavazi,ishara,wala maneno ya aina ya kampeni.
 Sikukuu hiyo ilipambwa na michezo mbalimbali ya watoto ,mnada,chakula na vinywaji.

 NA MUTAYOBA ARBOGAST,Bukobawadau,Missenyi
Next Post Previous Post
Bukobawadau