WATANO WAFARIKI DUNIA KATIKA MATUKIO TOFAUTI MKOANI MBEYA WAMO RAIA WA ETHIOPIA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi. |
Watu
watano wamefariki dunia Mkoani Mbeya katika matukio matatu tofauti
likiwemo la ajali ya haice iliyosababisha vifo vya watu wanne mkoani hapa.
Katika tukio la kwanza gari lenye namba za usajili T.519 Akh aina ya Toyota Haice ikiendeshwa na dereva asiyefahamika kugongana na pikipiki yenye namba za usajili T.535 Awc aina Ya T-Better eneo la Nanenane Jijini Mbeya.
Ajali hiyo imetokea Septemba 29
majira ya Saa 4 usiku katika eneo la Nane-Nane, Kata Ya Isyesye, barabara Kuu ya Mbeya/Njombe .
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ndugu
Ahmed Msangi amewataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa mwendesha pikipiki
ambaye bado jina lake halijafahamika sanjali na wengine watatu raia wa Ethiopia
ambao majina yao bado hayajafahamika mara moja ambao walikuwa wamepakizwa kwa pamoja
kwenye pikipiki hiyo kwa mtindo maarufu wa Mshikaki.
Aidha Katika ajali hiyo Edward Aloyce (42) Mkazi Wa Uyole ambaye
alikuwa abiria kwenye Haice alijeruhiwa
na amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu Msangi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari hiyo ya abiria pamoja na pikipiki hiyo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu Msangi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari hiyo ya abiria pamoja na pikipiki hiyo.
Amesema dereva wa hiace alikimbia mara
baada ya kusababisha ajali hiyo ambapo jitihada za kumsaka zikiendelea
kufanyika na jeshi hilo miili ya marehemu
imehifadhiwa Hospitali Ya Rufaa Mbeya.
Katika tukio jingine mtu mmoja Mkazi wa
Masoko Wilaya ya Rungwe Ndugu Tukupyelesya Enock Mwakifuna (54) amefariki
dunia mara baada ya gari walilokuwa wakisafiria T.913
Amb aina Ya Toyota Hillux ikiendeshwa na dereva asiyefahamika kuacha njia na kupinduka huko katika kijiji cha Masoko, Wilaya Ya Rungwe, Mkoa Wa Mbeya bararabara ya
Tukuyu/Lwangwa.
Aidha Katika ajali hiyo abiria Watatu wanawake
wawili na Na mwanaume mmoja walijeruhiwa na wamelazw katika hospital ya Hospitali ya Wilaya Rungwe huku chanzo cha .
ajali hiyo ni mwendo kasi dereva .
Kufuatia matukio hayo Kamanda wa Polisi Mkoa
Wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi Ahmed Msangi ametoa o wiito Kwa madereva kuwa Makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni
pamoja na kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza
Kuepukika.
mwisho