Bukobawadau

BALOZI KAMALA AENDELEA NA MIKUTANO YA KAMPENI NDANI YA KATA KASHENYE - NKENGE

Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala ,akiwahutubia wakazi wa Kata ya Kashenye katika mkutano wake wa Kampeni za kuwania Ubunge jimbo la Nkenge uliofanyika majuzi katika kijiji cha Bukwali-Kashenye Wilayani Missenyi.Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala ndiye balozi bora Afrika kwa mwaka 2015 nishani aliyoipata hivi karibuni Jijini Berlin Ujerumani kwa kuzingatia utendaji wake alipokuwa Waziri wa Afrika Mashariki, Mwenyekiti wa Mabalozi wa Afrika, Mwenyekiti wa Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pacific, na Balozi wa Tanzania Ubeligiji, Uholanzi, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya.
 Akiendelea kuwahutubia Wananchi na kuinadi Ilani ya CCM wakati wa Mkutano huo Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala amesema Mh Magufuli alikubali ombi lake na kuahidi kujenga barabara ya lami kutoka katoma hadi Kashenye pamoja na kujenga chuo kukubwa cha VETA Mkoni Kagera.
 Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala ameahidi kuchukua vijana 10 kutoka kila kijiji wakasome bure kwa gharama zake katika chuo cha Ufundi na anaendelea jitahada zake binafi za kuchangia kituo cha Afya ,zahanati iliyopo kijijini hapo
Pamoja na mambo mengine Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala  amesema serikali ijayo chini ya Magufuli  imedhamiria kujenga uwanja wa kimataifa katika eneo la Omkajunguti Mkoani Kagera ili kufungua usafiri wa anga.
Bwana  Lugemalila Magenge mwenezi wa CCM Tawi la Bushago Kijiji Bukwali
Mr Kagunguna akiimba shairi la kumsifu Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala
 Mzee Lugaibula akimpongeza Mr Kagunguna kwa shairi zuri lakuamasisha watu kumchagua
 Bwana Edwini Bukambu katibu wa siasa na Uenezi kata Kantigo
Mwenyekiti wa UWT na Mjumbe wa kamati kuu ya siasa Mkoa Bi Regnah Jovin
Bi Nora  akitolea jambo ufafanuzi
 Wataisoma namba, CCM mbele kwa mbele, waacheni waandamane ndivyo anavyo onekana....!
Mdau pichani anasema ' CCM ipo mioyoni mwa watu, wanaipenda na wanaiamini'
Sehemu ya Wananchi na Wana CCM wakiendelea kumsikiliza Mgombea wao Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala
 Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Missenyi William Katunzi akitolea jambo ufafanuzi na kuwaombea kura Wagombea wa CCM,Mzee Lugaibula kwa nafasi ya Udiwani wa Kata Kashenye,Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala nafasi ya Udiwani na Dr John Pombe Magufuli mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM 2015
 Mgombea Udiwani Kata Kashenye, Mzee Lugaibula akiwahutumia wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo  uliofanyika uwanja wa wazi jirani kabisa na nyumbani kwake
 Bwana Matunda pichani akifuatilia Mkutano huo
Mwendeshaji wa mkutano huo 'Mama Mboa ambae ni katibu wa CCM wa wilaya ya Missenyi
 Sehemu ya Wananchi wakifuatilia kwa umakini hutuba ya Mgombea jimbo la Nkenge, Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala wakati wa mkutano wake wa kampeni Kijijini Bukwali-Kashenye
  Wanachama wa CCM wakiwa katika hivi kuhudhuria  mkutano wa mgombea Ubunge wa CCM

Pale Sera za chama cha mapinduzi zinapo mkolea Kijana
 Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano huo
 Ndugu Babeye Mwenyekiti Umoja wa Vijana wa CCM, wilaya ya Missenyi akitema cheche
 Taswira Nyumbani kwa Mgombea Udiwani kata Kashenye Mzee Lugaibula
Mwisho anaonekana Ndugu Kitobelo Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya Missenyi
SEHEMU YA VIDEO YALIJIRI MKUTANO HUO
Next Post Previous Post
Bukobawadau