Bukobawadau

BALOZI KAMALA AFUNGA KAZI KATA ZA KITOBO NA RUZINGA : kufunga rasmi kampeni zake kesho Jumamosi Oct 24,Mjini Kyaka!!

MISSENYI OCT 23,2015:BALOZI DK.Diodorus Kamala ambaye ni mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Nkenge mkoani Kagera amesema Ilani ya chama chake imezungumzia kufuta kodi za mazao ambapo ameahidi kuwa akichaguliwa atalishawishi bunge kufuta ushuru katika zao la kahawa ili mkulima wa Kagera aweze kunufaika.
 Kamala alisema hayo jana katika mikutano yake ya kampeni katika vijiji vilivyomo kwenye kata za Kitobo na Ruzinga Wilayani Missenyi.
 Naye Ndugu Samuel Lugemalila meneja wa (Magufuli CLUB) Jimboni Nkenge akiomba kura za CCM kwa wananchi wa Bugandika kwa niaba ya Mgombea Ubunge wa jimbo la Nkenge kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Balozi DK.Diodorus Kamala AMESEMA ;"Balozi Kamala ameahidi kuwa endapo atachaguliwa, atajenga hoja na kulishawishi bunge kuangalia upya utaratibu wa kutoa mikopo kwa watoto waliosomea katika shule binafsi pindi wanapojiunga na elimu ya juu."
“Kusoma Private sio dhambia kwamba mtoto akifika elimu ya juu asipewe mkopo eti wazazi wake wana fedha nyingi,mzazi kumpeleka mtoto wake huku anatafuta elimu bora kwahiyo ni lazima tujenge hoja kupitia bunge kila mtoto apewe mkopo bila kujali kasoma wapi kwani watoto wote wanahaki hiyo”alisema Kamala 
 Wananchi wa Kata Bugandika wakiwa kwenye mkutano
 Ndg Willy Mutabuzi Mratibu Kampeni UVCCM na Shirikisho la Vyuo Vikuu Taifa Mkoani Kagera
Mdau Mpambanaji Charles Matunda katika moja ya harakati zake
Wazee wa Kijiji cha Bugandika wakifuatilia mkutano wa Kampeni
Ndugu Hamim Mahmudu Omary Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kagera akiwataka Wananchi na WanaCCM kukichagua Chama cha mapinduzi siku ya Jumapili Oct 25,2015.
Bango la Shule ya Msingi Ruzinga , Ulipo fanyika moja ya mikutano ya Balozi Dk.Kamala
 Umati wa watu katika mkutano wa Balozi Dk. Kamala
 Aidha Balozi Dk. Diodorus Buberwa Kamalaa ameendelea kuwaomba wanachi wajiunge na jamii ya CCM inayozidi kukua na kufanya kazi pamoja ,awataka wachague mafiga matatu, wamchaguwe Dk Magufuli , Balozi Dk. Diodorus Buberwa Kamala na Madiwani wa CCM ili kuhakikisha kazi ambayo imefanywa hadi sasa, na ambazo zinaendelea kufanya zinahakikisha maendelea na mafanikio ya Tanzania ya leo na vizazi vijavyo.
 Kibao hewani ni CCM mbele kwa mbele…., tumeipenda wenyewe…chaguo letu milele
 Ndivyo wanavyo onekana Wanahatunywi sumu hatujinyongi...CCM mbele kwa mbele, tumeipenda wenyewe, chaguo letu milele, nawavimbe wapasuke watajijua wenyee ,wakiwa  katika Vikao vya ndani ya Kata Kitobo
 Katika kumnadi Mgombea Udiwani wa Kata Bugandika  Ndg Hamody Ally Migeyo
 Kinyalyana Kinyashanani na tabasabu lake.
 Mwanadada Rahyuna, Kyaka moja  katika harakati zake za michakato ya Kampeni
 Tunawaomba Watanzania wote wenye sifa wajitokeze kupiga kura na kuyapokea matokeo kwa amani na Utulivu, kuna maisha baada ya Uchaguzi
 Mdau Samuel Lugemalila meneja wa (Magufuli CLUB) Jimboni Nkenge akisalimia na Bibi mwenye takribani miaka 115 rafiki wa Mama yake Mzazi pichani katikati, akifuatiwa na Mh.Hamody Ally Migeyo Diwani mtarajiwa wa kata Bugandika
Ndani ya kata ya Ruzinga tunakutana na tukio hili pichani


Next Post Previous Post
Bukobawadau