Bukobawadau

DK MAGUFULI AZIDI KUCHANJA MBUGA MWANZA KATIKA MAJIMBO YA MAGU, SUMVE, KWIMBA NA MISUNGWI

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni mjini Misungwi, Mwanza jana, ambapo aliwaomba wananchi kumpigia kura za ndiyo katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu.
 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Dk Magufuli akiingia kwenye gari baada ya kuhutubia akiwa juu ya gari mjini Ngudu, Kwimba leo
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akihutubia huku akiwa amesimama juu ya gari katika mkutano wa kampeni mjini Ngudu , wilayani Kwimba,, Mwanza, ambapo aliwaomba wananchi kumpigia kura za ndiyo katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu. 
 Dk Magufuli akiwahutubia wananchi waliouzuia msafara wake eneo la Mabatini, jijini Mwanza asubuhi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Msfara wa Dk Magufuli ukiingia eneo la Buzuruga jijini Mwanza ukielekea Wilayani Magu kuendelea na kampeni.
 Dk Magufuli akiwaomba wananchi wa Igoma jijini Mwanza asubuhi leo kumpigia kura za ndiyo katika uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu.
 Wananchi waliouzuia msafara wa Dk Magufuli wakiwa makini kumsikiliza  katika Kijiji cha Kisesa
 Mtoto akiwa amebeba  kiti alichokichukua nyumbani kwao ili aweze kusimama juu yake aweze kumuona vizuri Dk Magufuli katika Kijiji cha Kisesa
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Magu, Kiswaga wakati wa mkutano wa  kampeni mjini Magu, Mkoa wa Mwanza.
 Dk Magufuli akimvisha kofia bibi aliamua kuhamia CCM kutoka CUF wakati wa mkutano wa kampeni mjini Magu
 Dk Magufuli akijinadi kwa  wanananchi katika Jimbo la Sumve, wilayani Kwimba. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Dk Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Mgombea ubunge Jimbo la Sumve, Richard Ndassa Mganga, katika mkutano wa kampeni mjini Sumve leo.
 Wananchi wa Jimbo la Sumve wakimshangilia Dk Magufuli
  Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akihutubia huku akiwa amesimama juu ya gari katika mkutano wa kampeni mjini Ngudu , wilayani Kwimba,, Mwanza, ambapo aliwaomba wananchi kumpigia kura za ndiyo katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu.

 Mgombea ubunge Jimbo la Kwimba kupitia CCM, Mansoor Shanif akijiombea kura  yeye na Dk Magufuli katika mkutano wa kampeni mjini Ngudu Kwimba.
 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na ahadi alizokuwa akizitoa Dk Magufuli kwa wananchi wa Kwimba
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi wilayani Kwimba waliouzuia msafara wake
 Moja ya ujumbe uliokwepo katika mkutano wa kampeni  mjini Misungwi, Mwanza leo
 Wananchi wakishangilia kukubali kumpigia kura Dk Magufuli katika mkutano wa kampeni mjini Misungwi leo
 Katibu wa CCM Mkoawa Mwanza, Miradji Mtaturu akihamasisha wananchi wa Misungwi kumpigia kura Dk Magufuli
 Kundi la wasanii la Tumestuka walioamua kumpigia debe Magufuli wakifanya shoo katika mkutano wa kampeni  mjini Misungwi leo
 Aunt Ezekiel akielezea jinsi alivyoshtuka kwa kujitoa Ukawa na kujiunga na kundi la wasanii la Tumestuka linalompigia kampeni Dk Magufuli.
 Baadhi ya wasanii wa kundi la wasanii la Tumestuka wakifanya mazoezi ya Push Up wakati wa mkutano huo wa kampeni mjini Misungwi.
 MsaniiTausi  wa kundi la wasanii la Tumestuka wanaomuunga mkono Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni wilayani Misungwi, Mwanza
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, ambaye pia ni mratibu wa kampeni za Dk Magufuli, Abdallah Bulembo akiwananga wapinzani kwamba wasahau kabisa kwenda Ikulu, kwani Ikulu si mahali pa mchezo na itakuwa ni makosa makubwa kupeleka kiongozi Ikulu ambaye anafananishwa na Power Bank ya simu ambayo chaji yake ikiisha simu haichaji
 Mfano wa karatasi la kipigia kura la wagombea urais wa Tanzania Dk Magufuli na Makamu wake Samia Suluhu Hassan.
 Mgombea ubunge Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga akimuombea kura Dk Magufuli katika Mkutano huo. Pia alijiombea yeye na madiwani wa CCM.

Dk Magufuli akiwaaga wananchi wa Misungwi baada ya kumaliza mkutano PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
Next Post Previous Post
Bukobawadau