Bukobawadau

DK.MAGUFULI ASEMA WAPINZANI WANUNE, WACHEKE YEYE NDIYE RAIS 2015, AMFAGILIA NAPE MTAMA

 Mgombea urais wa Tganzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Mtama, ambaye pia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye mjini Mtama leo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

Akihutubia mjini Mtama, amesema kuwa Wapinzani Wanune, Wacheke yeye ndiye Rais 2015 na atahakikisha anafanya kazi kwa kuwaletea mafanikio watanzania.
 Moja ya mabango katika mkutano wa kampeni mjini Mtama
 Mgombea ubunge Jimbo la Mtama, Nape Nnauye akimuombeakwa Wananchi  kura za ndio  katika mkutano wa kampeni mjini Mtama
 Dk Magufuli akifurahi wakati Nape Nnauye akimmwagiua sifaa za kufaa kuwa rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mkutano wa kampeni mjini Mtama.
 Warembo wafuasi wa CCM wakitabasamu huku wakiwa wamejiremba wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Mpilipili mjini Lindi leo.

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mke wa Rais, Salma Kikwete akimuombea kwa wananchi  kura za ndiyo Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Mpilipili mjini Lindi leo.  PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
 Mfano wa karatasi la kupigia kura likionesha jinsi watu wanavyotakiwa kumpigia kura za ndiyo Mgombea wa Tanzania kupitia CCM, Dk Masgufuli na mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo.
 Dk Magufuli akihutubia wananchi katika Mji wa Nachingwea Asubuhi saa 2;30 katika mkutano wa kampeni
 Wananchi wa Nachingwea wakisashangilia baada ya kufurahishwa na ahadi za Dk Magufuli kwao.
 Wananchi wakinyoosha mikono kukubali kumpigia Dk Magufuli na Mgombea ubunge Jimbo la Nachingwea, Hassan Massala PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
 Dk Magufuli akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Nachingwe wakati wa mkutano wa kampeni mjini Nachingwea leo asubuhi.
 Dk Magufuli akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Ruangwa wakati wa mkutano wa kampeni mjini Ruangwa leo.
 Baadhi ya kadi zilizorudushwa na waliotoka upinzani, akiwa zimesambazwa baada kutangaza kujiunga na CCM wakati wa mkutano wa kampeni mjini Ruangwa.
 Mmoja wa waliokuwa wanachama wa upinzania akielezea mbele ya Dk Magufuli sababu zilizomfanya aihame CUF na kujiunga na CCM  wakati wa mkutano wa kampeni mjini Ruangwa leo. Moja ya sababu alizozitoa ni kwamba ni chama cha uhuni na fujo pia hakijaweka mgombea urais.
 Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Lindi, Mzee Ali Mtopa akifungua mkutano wa kampeni kabla ya kumkaribisha kujinadi Dk Magufuli
 Mmoja wa wananchi Jimbo la Mtama akiwa amejichora kichwani neno CCM
 Msanii Ali Kiba akitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni mjini Mtama
 Dk Magufuli akisalimiana na Msanii Ali Kiba
 Dk Magufuli akiunguruma katika Jimbo la Mtama ambapo alimnadi Nape Nnauye kwa kuwaambiwa wananchi wasije wakafanya makosa kutompigia kura za ndiyo Nape ambaye alimwita kuwa ni mpiganaji jasiri na hapendwi na mafisadi kwa sababu anapingana nao waziwazi.
 Jisomee mwenyeeeeeeeeeee
 Dk akimwagia Nape sifa lukuki kwa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni Jimbo la Mtama
 Wananchi wa Jimbo la Mtama wakinyoosha mikono ikiwa ni ishara ya kukubali wakuwapigia kura za ndiyo Dk Magufuli na Nape wakati wa mkutano wa kampeni Jimbo la Mtama, mkoani Lindi.
 Ni furaha iliyoje kwa wakazi wa Mtama
 Dk Magufuli akimvisha kofia aliyekuwa dereva wa Mgombea ubunge Jimbo la Mtama kupitia Chadema, Seleman Mathew, baada ya kutangaza kuchana na chama hicho na kujiunga na CCM katika kiutano wa kampeni Jimbo la Mtama.

 Wasanii Temba na Chege wakifanya vitu vyao wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Mpilipili mjini Lindi leo
 Dk Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais, Salma Kikwete wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Mpilipili. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, ambaye pia ni Mratibuwa Kampeni za Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli (katika), Abdallah Bulembo.
 Yamoto Band akitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni mjini Lindi
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akimpigia kamnpeni Dk Mgufuli wakati wa mkutano wa kampeni mjini Lindi leo.
 Sehemu ya umati wa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni za CCM mjini Lindi leo.
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi mjini Lindi leo
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Lindi Mjini,Hassani Kaunje
 Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa akitumbuiza wakati wa mkutano huo
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Ali Mtopa akicheza taarabu hiyo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
Next Post Previous Post
Bukobawadau