LOWASSA AWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA AJIRA ZITOLEWAZO NA AFRIKA MASHARIKI
WATANZANIA wametakiwa kujifunza kuchangamkia fursa za ajira zinazotolewa na Afrika Mashariki kama ilivyo kwa nchi nyingine.
Kauli hiyo ilitolewa jana na mgombea wa Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa alipokuwa kwenye kampeni zake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Namanga.
Lowassa alisema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atahakikisha kuwa watanzania wanachangamkia fursa za Afrika Mashariki kama ilivyo kwa Kenya.
"Napenda mahusiano ya Afrika Mashariki yawe ya kweli na siyo upande mmoja unafaidi na mwingine haufaidi,"alisema na kuongeza kuwa:
"Watanzania wakiwa wanapita kwenye mpaka wa Namanga wasisumbuliwe wapite bila shida."
Sehemu ya wananchi wa eneo la Kisongo, Jijini Arusha wakiwa wamefunga barabara kuzuia msafara wa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, ili waweze kumsalimia na kumsikiliza, wakati alipokuwa njiani kuelekea eneo la Ngaramtoni mpaka Namanga, kwenye Mkutano wa Kampeni, leo Oktoba 7, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, ARUSHA.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwa vijana wa eneo la Kisongo, walipokuwa wakimsindikiza mpendwa wao.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Mringa, Jimbo la Arumeru Magharibi, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Jimbo la Arumeru Magharibi waliohudhulia Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Mringa, Jimbo la Arumeru Magharibi, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Arumeru Magharibi katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Mringa, Jimbo la Arumeru Magharibi, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Jimbo la Longido waliohudhulia Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa Namanga, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwasalimia watoto walikuwepo kwenye Mkutano huo.
Lowasaaaaa...... Mabadilikoooooooo......
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwasalimia wananchi wa Mji wa Namanga, katika Jimbo la Longido, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Namanga, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Namanga, Jimbo la Longido, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Namanga, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015. Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido kupitia Chadema, Onesmo Ole Nangole, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Namanga, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.
Zawadi: Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akionyesha kwa wananchi zawadi iliyotolewa na Vijana wa Mji wa Namanga kwa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa.
Burudani ya Asili ya Kimaasai.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiteta jambo na aliewahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani katika Serikali ya Kenya, Mzee John Keen, aliefika eneo la Namanga kuhudhulia Mkutano wa Kampeni zake, leo Oktoba 7, 2015.