MKUU MPYA WA WILAYA YA NGARA MKOANI KAGERA AAPISHWA RASMI NA MKUU WA MKOA WA KAGERA
Mkuu mpya wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bi Honoratha Chitanda aliapishwa rasmia na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Kagera Mhe. Johna Mongella kushika wadhifa huo wa kuiongoza Wilaya ya Ngara na kukabidhiwa rasmi nyaraka mbalimbali za kumsaidia kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Bi Honoratha Chitanda Mkuu mpya wa Wilaya ya Ngara aliapishwa Agosti 12, 2015 katika hafla fupi iliyofanyka katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera na kuhudhuriwa na viongongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wananchi.
Mara baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Ngara Bi Honoratha Chitanda alisema atatekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ili kumwakilisha Mhe. Rais vyema katika Wilaya hiyo.
Aidha Bi Chitanda alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete kumwamini na kumteua pia kuwa na imani naye kama mama kwani na akina mama wanaweza kutekeleza majukumu mbalimbali kama walivyo wananume.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John
Mongella alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ngara Bi Chitanda kwa kuteuliwa na
kusistiza kuwa jukumu la kuteua wasaidizi wake ni la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
yeye mwenyewe na anapoona inafaa kufanya hivyo.
Bi Honoratha Chitanda kabla ya
kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara alikuwa
mstaafu katika wadhifa wa Umakamu
wa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) tangu Mei 2015. Na kabla ya
kuteuliwa kwake Wilaya ya Ngara ilikuwa inaongozwa na Bw. Costantine Kanyasu
aliyeachia wadhifa huo kwa kugombea ubunge Jimbo la Geita Mjini.
Katika picha ya pamoja