Bukobawadau

NEC yasema iko katika hatua ya mwisho ya kuboresha mfumo wa matokeo ya uchaguzi.

Tume ya taifa ya uchaguzi NEC iko katika hatua za mwisho za kuboresha mfumo wa matokeo ambapo ukimalizika vyama vya siasa vitaitwa kukagua na ikiwezekana wakae zaidi ya siku moja kufuatilia namna utakavyofanyakazi.
Mkurugenzi wa uchaguzi wa NEC Bw Ramadhani Kailima ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wahariri wa habari ambapo amevitaka vyama vya siasa kutokukimbilia kulalamika vitumie kanuni za maadili kuwasilisha malalamiko yao badala ya kwenda kwenye vyombo vya habari.
Mwenyekiti wa tume hiyo jaji mstaafu Damian Lubuva ameendelea kusisitiza vyama vya siasa kutokuhamasisha wananchi kubaki vituoni baada ya kupiga kura ili kuepusha vurugu ikiwa ni pamoja na wagombea ngazi zote kukubali matokeo na kuzingatia maadili ili zoezi limalizike kwa amani.
Baadhi ya wahariri walioshiriki mkutano huo mbali na kueleza changamoto wanazokabiliana nazo katika kuhariri habari za kampeni wamesema kuna haja ya tume kuendelea kukumbusha makundi yote ambayo ni wadau wa uchaguzi namna ya kushiriki mchakato wa kampeni, kupiga kura hadi kutangazwa kwa matokeo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau