Kigosi ameyasema hayo alipokuwa katika moja ya mikutano inayoendeshwa na kundi la wasanii lenye kauli mbiu ya Nimestuka, katika jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kundi hilo inayopita kijiji kwa kijiji katika kuhakikisha kwamba wanawaelimisha vijana wenzao kuhusiana na usikilizwaji wa sera na mapokeo ya demokrasia kwa jamii.
Awali akiongea kabla ya kuwakaribisha wenzake 12 alioandamana nao, Kigosi amesema yeye alipokuwa Ukawa alikuwa akishuhudia vijana wakihamasishwa kupinga hata mambo yanayoonekana kuwa na tija yaliyofanywa na seriikali jambo ambalo yeye mwenyewe aliliona kuwa ni upotoshwaji wa wazi wazi.
"Naamini kuwa mpinzani, sio kupinga kila kitu, walipaswa pia kutufundisha jinsi ya kukabiliana na maisha kama vijana, lakini nikaja kugundua nimekosea sana kuacha kuungana mkono na Magufuli", alikiri Kigosi.
PICHANI JUU: Msanii wa filamu Ndende, akihamasisha wananchi wa Kishapu kuhusiana na kumuunga mkono mgombea wa Chama cha Mapinduzi, Dk John Pombe Magufuli