SHAIRI :WAZALENDO – 2015
WAZALENDO – 2015
1)
AWAMU
YA TANO NDO HII, VIONGOZI KAMPENINI
TWAMUHITAJI
SAHIHI, WALA SIO WA UTANI
HAPA
HAKUNA KUWAHI, SAFARI HII TUKO MAKINI
BIBLIA
QUR’AN, VIAPIE UKO MAKINI.
2)
SAFARI
HII TUMECHOKA TWAWATOLEENI UVIVU
SISI
TUNAWAAMINI, NDO MAANA TWAWAPA SHAVU
KURA
TUKIWAPIGIA, ILI MUWE WASIKIVU
KISHA
MNATUGEUKA, KUTUONA WAPUNGAVU.
3)
USO
KWA USO TU LIVE NA IMANI ZENU POTOVU
KWA
NINI MWANG’ANG’ANIA, MPAKA MUWE VIONGOZI
HAPO
HAPO KUNA SIRI, NDO MAANA MWAOTA SHAVU
SISI
TUNADHOOFIKA, NYIE MWAZIDI KUNONA.
4)
IMEKUWA
SIKU NYINGI, WAZALENDO TWATESEKA
WALO
FAIDI KWACHACHE WENGI TUMESAHAULIKA
RUSHWA
KOTE IMETAWALA, MASIKINI HANA HAKI
NJOO
UTOE UCHAFU, TANZANIA IACHE NUKA.
5)
NYIE
WATU MMEROGWA, MWAHITAJI KUOMBEWA
DUNIANI
KUWA BINGWA, MKASAHAU AKHERA
HAMUOGOPI
ULINZWA, NCHI MLIONGOZAJE
TAMAA
MWAWEKA MBELE, UMAUTI WENU NYUMA.
6)
SASA
UMEKUWA MCHEZO, UONGOZI KUGOMBEA
PESA
MNATUMWAGIA, KISHA MNATUNYAKUA
MIDOMO
MMETUGUNGA, HATUWEZI FURUKUTA
MWALIMU
ALITUONYA, MKWEPWE KAMA UKOMA.
7)
MWAMWAGA
PESA HADHARANI, BILA HATA YA KIFICHO
HAYA
ZIMWEKURUKENI, KANA KWAMBA HATUNA MACHO
HII
SASA SI SAISA, NI YA MWENYE KUWA NACHO
KWA
MIPANGO YA MANANI, ATAPITA ALOMPANGA.
8)
HATUHITAJI
MAPESA KILIO CHETU USAWA
ATACHO
PEWA MENEJA NA MKULIMA IWE SAWA
SIO
MWENYE KUTUUMA-NA KUPULIZA KAMA PANYA
KUTUACHA
NA BUTWAA – JINSI ATAKANYOTUNYONYA.
9)
TWAWAONYA
WAZALENDO, WENYE AKILI TIMAMU
TUACHENI
KUPUMBAZWA – NA WAUCHU WA UONGOZI
ANATUPIA
TUKANGAA – NA AHADI ZA UONGO
MGOMBEA
WA KUHONGA – AKIFIKA IKULU NI SUMU.
10)
TUMKUNJENI
SAMIKI, BADO ANGALI MBICHI
WALE
WEZI WA ZAMANI, SISI HATUWA SADIKI
FISADI
HUWA HASIKII, NA WIZI WAKE AACHI
MWIZI
SISI HATUMTAKI, WACHA TUMEACHE BENCHI.
11)
JAMANI
SISI TUMECHOKA, MWENYEZI MUNGU SHAHIDI
KIONGOZI
TUNAETAKA JULETUTAE FAIDI
WATUFANYA
BURICHEKA, KWAMUOGOPI WADUDI
WAJIONA
WAMEFIKA, HWA MOLA HAWATORUDI.
12)
KWA
MANANI TUMEOMBA TUNASUBIRI NUSURA
YEYE
PEKEE NDO MUUMBA AATAELETA NUSURA
NA
HAWA NDO KAWAUMBA INGAWA SI WATUKERA
TUNAKUOMBA
RABUKA, TUKINGE NA SHARI ZAO.
12A)
MZALENDO SI MGENI NJOO MWENYEJI AHAME
WAMEBAKIRI
KAULI, NJOO MWENYEJI AHAME
KUMUHIMISHA
MWENYEJI, UKAMFADHIRI MGENI
JAMANI
HII NI DHURUMA, ISO KUWA NA MFANO.
13)
SIO WOTE NI WACHAFU WAPO WENGINE WASAFI
WAO NI WAADILIFU, HAWA SIO MABEPARI
HAWANA HATA KASIKENDO WANA SIKIKA KWA WEMA
KURA ZETU TUWAPE LEO, KESHO NASI TUFURAHI.
14)
TWAHITAJI
MWANDIRIFU, MWENYE MOYO WA IMANI
ATAE
ONDOSHA MACHAFU, NA KUENDELEZA MEMA
KWA
MOLA AWE NA HOFU, AJUWE WAJIU WAKE
MWENYE
ROHO SIO CHAFU, NA KUWAJALI WENZAKE.
15)
TWAHITAJI
MWANADAMU, HAIJARISHI CHAMA GANI
AMBAE
HANA HASIRA, KUTUTIA UTATANI
WALA
SI KING’ANG’ANIZI, ASO KUBARI KUSHINDWA
ASIYE
TAKA MAKUU, AJIWEKA KAWAIDA.
16)
HAIJARISHI
DINI GANI, ILI MRADI ANA IMANI
IKIWA
NI MCHA MUNGU, SISI TUTAPATA AMANI
SI
MBAGUZI WA DINI, KABILA AU HALI GANI
ATAEJALI-MAENDELEO
YA WANACHI NCHINI.
17)
TUNASISITIZA
UUTU- KWA HUYU MPYA KIONGOZI
ATAMBUE
NASI WATU, ASUTIE SIMANZI
AJUE
HAPA NI KWETU, SI TU KWA AKINA FULANI
WAZALENDO
TU NYUMBANI, HAPA SIO UGENINI.
18)
KUMBUKA
ALOKUPA CHEO, NI MWENYEWE MTUKUKA
TUFANYIE
UWADIRIFU, ASIJE KUKASIRIKA
USIJE
KUWA KINYONGA, NA KUGEUKA KUWA NYOKA
KAMWE
HATUTOKUWEZA SHAHIDI ATAKUBUKIKA.
19)
TWASHITAKI
KWA MUUMBA, RAIS WETU SHAHIDI
VITUKO
VYA MAFISADI, TANZANIA VIMEZIDI
WAMEGEIZA
SIASA, KITENGO CHA UFISADI
UKIINGIA
IKULU – WEKA MAGUFURI WASIRUDI.
19A)
HII DEMOKRASIA – SI NCHI YA KISURUTANI
AWAMU
HII YA TANO SIO YA KURISHANA
TUSHAMUONA
MSAFI SISI TOKEA ZAMANI
YEYE NDO CHAGUO LETU WALA HANA MPINZANI.
19B)
MWENYE AKILI AFIKIRIE TUSICHEZEE BAHATI
ALOTUPAPELI
AWAKI-ATUTOBOA JICHO KWA KIJITI
MWIZI
HATA ASUGULIWE KWA JIKI WALA HATAKATI
NAMCHAGUA
MSAFI, FISADI KULA YANGU HAPATI.
20)
ONA
HAWA MAFISADI KUTUFANYA PUNGUWANI
TANGU
LINI MTU UIBE NA UFUKUZWE KAZINI
WEWE
WEWE TENA URUDI, ETI USHIKE USUKANI
HIKI
JAMANI NI KIOJA CHA KARNE DUNIYANI.
21)
MAFISADI
MIAKA YOTE HULA WAO PEKE YAO
SAFARI
HII WATUZUGA ETI NASI TULE NAO
HII
NI DANGANYA TOTO, TUMEJUA MBINU ZAO
TUNAMTAKA
MSAFI, ALOMESH HILA ZAO.
22)
KUNA
TOFAUTI KUBWA TAJIRI NA MASIKINI
ZAMANI
WASHAPUUZWA HAWAJUI WALA NINI
FISADI
NA MATAJIRI KULA YAO MOJA SAHANI
HAWAHITAJI
RAIYA WAO HUTEMBEA ANGANI.
23)
WAMESHUKA
ONBA KURA TENA KWA KUHONGA PESA
UTAJIRI
WAKINADI ETI NI WANA SIASA
HALI
HII WALIPITA CHA MOTO TUTAKIONA
MOLA
ATUPISHE MBALI IKULU WASIINUSE.
24)
RAIS
ASIINGILIWE KATIKA MAAMUZI YAKE
TARATIBU
AZIPANGE KUTIMIZA AHADI ZAKE
AKIHITAJI
USHAURI BILA SHAKA ATAKWETENI
ILA
MSIMVURUGE NA ROHO ZENU ZA KWANINI.
25)
UKISIKIA
RAIYA, AHITAJI MSAADA
HARAKA
MTUMIZIE, UONDOE YAKE SHIDA
MA
WEWE IKIMPUUZA ATAKOSA HATA PAWENDA
JOHN
JALI MZALENDO NA SISI TUTAKUPENDA.
26)
USIFANYE
TUJUPENDE MPENDEZE MOLA WAKO
ALO
KUPA HICHO CHEO, NA HIZO PUMZI ZAKO
UONGOZI
ALISHA TAJA, NASI TUWE NYUMA YAKO
SASA
TUFANYIE WEMA, ASIJE KUCHAPA VIBOKO.
27)
PENDELEA
MASIKINI UFUKARA HAKUUOMBA
FISADI
ALIMUWAHI PESA ZOTE AKAKOMBA
TANZANIA
ITAJIRI HAIITAJI OMBA OMBA
RAIS
KILA LA KHERI NYUMA SI TWASHIRI KAMBA.
28)
RAIS UJITOLEE
KUWEKEZA VIJIJINI
HUKO
WAMEWAPUUZA KANA KWAMBA SI NCHINI
MASIKINI
WANYAMAZA NA HAWAJUI KUNA NINI
UKIMYA
WAO SI BURE ISIJE KUWA WA LAANI.
29)
BARA
PIA VISWANI – NI MUUNGANO WA NCHI MOJA
WAZALENDO
HAPA NCHINI, SISI NI KITU KIMOJA
BARA
TWATAKA RIDHIKA, PEMBA MPAKA UNGUJA
RAIS
WA MUUNGANO NDO HUYO TUNAMMGOJA.
30)
THEHEBU
KUBWA NI MBILI WAKRISTO NA WAISLAM
WOTE
TUHESHIMUMIANE NA KUPEANA SALAAM
NJE
WANATUTAMANI, TUNAVYOISHI KWA SALAMA
MFANO
WA JIJI LETU, BANDARI YA SALAMA.
31)
ELIMU
KWETU MUHIMU MAVAZI PIA MAKAZI
TUTIBIWE
KIRAHISI TUYAPATAPO MARADHI
AJIRA
ZIWE KWA WINGI, NASI TUSHIRIKI KAZI
USALAMA
UBORESHWE KUKOMESHA MAJMBAZI.
32)
MSAFI
TUMAKUOMBA ZIDISHA ZAKO JUHUDI
TANZANIA
ISAFISHE UUTUTE UFISADI
MAFISADI
WASHATOKA, UZUIE WASIRUDI
SIFA
YETU YA ANAMI, TUUMBE MUNGU IRUDI.
33)
MACHAFUKO
TUYAKWEPE, KWANI VITA HAINA MACHO
MIFANO
TUNAIONA, KWANI HAINA KIFICHO
WENZETU
WANAUWANA HAWANA PA KUJIFICHA
IKIANZA
IMEANZA, KAMWE HAIWEZI ACHA.
34)
TWAWAONYA
MAJIRANI WASIO JALI AMANI
KWAMBA
TOKEA ZAMANI, TUMEITUNZA AMANI
TUNACHOLINDA
AMANI, BARA MPAKA VISIWANI
TANZANIA
YA AMANI, JADI YETU NI IMANI.
35)
TUNAINUA
MIKONO MOLA ASISHUSHE GHARIKA
UONEVU
UKIZIDI – WOTE SI TUTADHURIKA
YEYE
PEKEE NDO ANA SIRI HUKUMU YAKE IKIFIKA
TUSHIKANE
KWA MAOMBI MUNGU ATATUITIKA.
36)
TUNAINUA
MIKONO KUOMBA KWAKO RABUKA
HATUNA
SI KIMBILIO, ILA KWALO MTUKUKA
RABBI
ONDOA VILIO, WAZELENDO TWATESEKA
TUTUNUKU
KIONGOZI NA SISI TUPUMZIKE.
37)
TUMIMINIE
BARAKA ISAMBAE DUNIANI
ISITOKEE
GHARIKA , KUJA KUTUANGAMIZA
TUACHE KUTENDA DHAMBI, TUMUOGOPE MANANI
TUWE
WATU WA UPENDO UTUKINGE NA SHETWANI.
38)
NIMEZALIWA
TANZANIA NIMEKULIA TANZANIA
MIMI
NAJIVUNIA KUITWA MTANZANIA
NAPIGANIA
NCHI YANGU, SWEET HOME TANZANIA
MOLA
TUSHUSHIE NEEMA – TANZANIA YA WATANZANIA.
UTENZI
HUU WA WAZALENDO NI ZAWADI KWA RAIS WETU MSAFI,
MPENDWA,
MTARAJIWA. EWE MOLA WETU TUALALIE UCHAGUZI 25/10/2015 UWE WA SALAMA NA AMANI.