SHIGONGO ATOA SEMINA YA UJASIRIAMALI KWA WANACHAMA WA TCRA SACCOS
Eric Shigongo akifundisha somo la Sheria 10 zilizothibitishwa za jinsi ya kutoka kwenye umasikini hadi mafanikio kwa wanachama wa TCRA Saccos.
Baadhi ya wafanyakazi na wanachama wa TCRA Saccos wakimsikiliza kwa makini somo la Shigongo.
Shigongo akizidi kutoa semina kwa wanachama wa TCRA Saccos.
Mwenyekiti wa TCRA Saccos, Erasmus Mbilinyi akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Ally Yahaya Simba ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika semina ya leo.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Ally Yahaya Simba akitoa nasaha zake kwa wanachama wa TCRA Saccos.
Wanachama wa TCRA Saccos wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Ally Yahaya Simba.
Eric Shigongo (kushoto) akifurahia jambo wakati Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Ally Yahaya Simba akitoa nasaha zake.
Mmoja wa wanachama wa TCRA Saccos akitoa shukrani kwa Shigongo baada ya kulielewa vizuri somo lake.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Ally Yahaya Simba akisoma mojawapo ya vitabu vya Shigongo.
...Hapa akiangalia CD ya Shigongo.
Shigongo akiweka saini yake katika vitabu vilivyonunuliwa na wanachama wa TCRA Saccos.
Wanachama wa TCRA Saccos wakinunua CD na vitabu vya Shigongo baada ya semina.
Shigongo akibadilishana mawazo na wanachama wa TCRA Saccos.
MWANDISHI na mhamasishaji mahiri Afrika ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo James, leo ametoa semina ya ujasiriamali kwa wanachama wa TCRA Saccos.
Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini Dar es Salaam.
Katika semina hiyo, Shigongo amefundisha somo la Sheria 10 zilizothibitishwa za jinsi ya kutoka kwenye umasikini hadi mafanikio.
Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Ally Yahaya Simba ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi alieleza umuhimu wa kuwa na Saccos katika kuinua maisha ya wanachama wake. Baada ya semina hiyo kumalizika, wanachama wa TCRA Saccos walipata fursa ya kununua vitabu pamoja na CD za Shigongo zilizokuwa zikiuzwa eneo hilo.
(HABARI; CLARENCE MULISA, PICHA; PATRICK BUZOHERA / GPL)