TAARIFA YA HIVI PUNDE AJALI YA HELKOPTA
Mgombea ubunge jimbo la Ludewa kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Deogratius Filikunjombe, rubani na abiria wengine wote wamekufa baada ya helkopta kuanguka na kuteketea katika hifadhi Selou. >>> Jeshi la Polisi pamoja na Bunge limethibitisha leo mchana kutokea ajali hiyo mbaya na miili ya marehemu inasubiriwa uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.