Bukobawadau

UNCLE SAM NA KAMPENI ZA LALA SALAMA JIMBO LA NKENGE (Operation Tokomeza Ukawa )

Ndugu Samuel Lugemalila kampeni meneja wa (Magufuli CLUB) Jimbo la Nkenge akiendelea kusaka kura za wagombea wa CCM Mtaa kwa mtaa, chocho kwa chocho ,kijiji kwa kijiji huko Missenyi,kama anavyo onekana pichani akiwahutubia wananchi wa Kijiji Bubalebwela kata ya Kilimilile iliyoko wilayani Missenyi na kuwataka wananchi hao kuwapuuza Wapinzani
Katika harakati hizo maarufu kama (Operation Tokomeza Ukawa ) Ndugu Samuel  amemuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dk Magufuli na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dk. Diodorus Buberwa Kamala pamoja na Diwani mtarajiwa kata ya Kilimilile Bi Letcia Pascal
 Wananchi wakimsikiliza Ndugu Samuel Lugemalila alipokuwa akiwahutubia jioni ya jana kwenye mkutano wa Kampeni (Operation Tokomeza Ukawa )
 Pichani kulia ni mgombea Udiwani  kata ya Kilimilile Bi Letcia Pascal
 Wananchi wakiendelea kufuatilia hutuba mbalimbali  katika mkutano uliofanyika jioni ya jana

 Ndugu Seka Abdulmalik wa Mutukula akitema Cheche katika mkutano huo
 Wakazi wa Kata Kililimile wakiendelea kufuatilia mkutano huo
 Kikosi kazi maalum kwa ajili ya kutafuta kara za Wagombea wa CCM Wilayani Missenyi
Pichani kulia ni  Bwana Swalehe Amis  mwenyekiti wa CCM kata Kilimilile akibadilishana mawazo na Uncle Sam muda mchache kabla ya mkutano huo kuanza
Taswira mbalimbali (Operation Tokomeza Ukawa ) 
Next Post Previous Post
Bukobawadau