Bukobawadau

WATANZANIA WATAKIWA KULINDA SHAHADA ZAO ZA KUPIGIA KURA

 Wakazi wa mji wa Singiga na vitongoji vyake wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kuwaomba wampigie kura za ndio ifikapo Oktoba 25 Mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu wa Urais,Wabunge na Madiwani.
 Harakati za kusaka nafasi ya juu  ya uongozi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo zimepiga kambi mkoani Singida kwa mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt John Pombe Magufuli pichani kuwahutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika uwanja wa Pipoz mjini humo kwenye mkutano wa kampeni.

Dkt Magufuli ameishauri tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kutimiza wajibu wake wa kutenda haki kwa wagombea wote wa ngazi za Uraisi,pia amewataka Wananchi wakatae kulaghaiwa na baadhi ya watu wanaotaka madaraka kwa nguvu,kwa kuzinunua shahada zao za kupigia kura,badala yake amewaomba wazitunze shahada hizo ili ifikapo Oktoba 25 mwaka huu wapige kura. PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA
 Maelfu ya Wananchi wa Singida wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia na kujinadi kwa kuwaomba ridhaa ya kuwaongoza iwapo watamchagua kuwa Rais ifikapo Oktoba 25 mwaka huu,kwenye uchaguzi mkuu,Dkt Magufuli amewaomba wananchi hao alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Pipoz,mjini Singida.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi,Dkt Joh Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Singida mjini Mussa Sima mbele ya maelfu ya Wananchi (hawapo pichani) kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Pipoz mjini Singida jioni ya leo.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Iramba Magharibi kwa wakazi wa Iramba mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara,mara baada ya kumkabidhi Ilani ya chama hicho.
 Wananchi wakiwa wamefunga barabara wakizuia msafara wa Mgombea Urais Dkt John Pombe Magufuli katika kijiji cha sepuka na Ndago,wakati msafara huo ukielekea Iramba kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwigulu Nchema kabla ya mkutano wa hadhara wa kampeni kuanza mjini Kiomboi,wilayani Iramba.
 Mgombea Ubunge wa jimbo la Iramba Magharibi,Mwigulu Nchemba akiwahutubia wananchi wa Kiomboi mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni.
Baadhi ya Kadi za Wanachama wa Chadema zilizokabidhiwa kwa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Kiomboi,Wilayani Iramba mapema leo mchana.
Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukikatiza katika bonde la mto Sibiti kupitia barabara ya Nduguti kuelekea wilayani Mkalama,kwenye mkutano wa kampeni mapema leo mchana.
  Ujenzi wa Daraja la Sibiti wilayani Mkalama likiwa katika hatua za mwisho kukamilika,Daraja hilo limeleta matumaini mapya kwa wakazi hao wa Mkalama,kwani wakati wa mvua ilikuwa ni kikwazo kikubwa kwao wakati wa kusafiri na hata kusafirisha mazao yao ya biashara.
 Wakazi wa kijji cha Mtinko wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,aliposimama na kuwasalimia.
Wakazi wa kijiji cha Mtinko wakiwa wamefunga barabara wakitaka Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli awasikilize shida zao ili akiingia madarakani aweze kuwasaidia
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Ilongero,Singida Vijijini mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni.
 Wananchi wa Singida na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa People's,mjini Singida katika mkutano wa kampeni wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kabla ya kuanza kuwahutubia jioni ya leo.
   Mjumbe wa Kamati ya Kampeni CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba akiwaomba wakazi wa mji wa Singida na vitogoji vyake waliofurika kwenye mkutano wa kampeni,kuwa ifikapo Oktoba 25 mwaka huu wajitokeza kwa wingi kumpigia kura za ndio za kutosha Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na Mbunge na Madiwani ili wapate ushindi wa kishindo. 

  Mjumbe wa Kamati ya Kampeni CCM,Ndugu January Makamba akimuombea kura za kutosha mmgomea Urais wa CCM Dkt Maguli pamoja na Mbunge na Madiwani wa Singida mjini kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Pipoz mjini humo.
Baadhi ya Kadi za Wanachama wa Chadema zilizokabidhiwa kwa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Kiomboi,Wilayani Iramba mapema leo mchana.
 Maelfu ya wakazi wa Singida wakiwa kwenye mkutano wa kampeni za Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,uliofanyika katika uwanja wa Pipoz mjini humo.
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mjini (Mbunge Mstaafu),Mohamed Dewji akimwombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa Singida na vitongoji vyake katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Pipoz,mjini Singida,Dewji pia ametangaza kumuunga mkono aliyemrithi kiti chake cha Ubunge,Ndugu Mussa Sima.
Next Post Previous Post
Bukobawadau