Jameson yaandaa pre-party George and Dragon Dar kuelekea Jameson Live Party itakayofanyika Nairobi.
- Mshindi mmoja kujishindia
tiketi ya watu wawili kwenda Kenya kwenye party ya Jameson
itakayotumbuizwa na B.O.B
Jameson inaandaa pre-party
itakayofanyika tarehe 21 ya mwezi huu katika bar ya George and Dragon jijini
Dar es Salaam.
Watumiaji wa Jameson
watakaonunua chupa ya kinywaji hicho watafanikiwa kuingia moja kwa moja kwenye
droo ya kushinda tiketi ya kwenda Kenya kushuhudia party ya Jameson itakayofanyika
hapo tarehe 12, December.
Jameson Live 2015 Party,
inamleta msanii wa hiphop kutoka Marekani, Bobby Ray Simons, maarufu kama
B.O.B, ambayo itafanyika Ngong Racecourse hapo tarehe 12 December.
Rapa huyo mzaliwa wa Atlanta
amezungumzia kuhusu show yake hiyo ya Nairobi katika ukurasa wake wa Facebook,
akiwataka mashabiki wake wajiandae kwa show kali.
B.O.B ambaye alitambulika katika
ulimwengu wa muziki kupitia kupitia mixtape yake ya Cloud 9, amefanikiwa kufanya
show sehemu mbalimbali duniani huku wimbo wake wa ‘Airplanes’ na ‘Nothing on
You’ aliyomshirikisha Bruno Mars zikiongoza chati mbalimbali za mziki duniani.
Nyimbo zake za hivi karibuni kama ‘So Good’ na
‘Headband’ nazo zimefanikiwa kumfanya B.O.B kuwa mmoja ya wanamuziki wakubwa
duniani.
Huku akiwa ameshinda tuzo mbalimbali za BET, MTV
pamoja na Teen Choice na huku akifanikiwa kuchaguliwa kuwania tuzo za Grammy
zaidi ya mara sita, B.O.B ameshawahi kufanya show na wanamuziki mahiri kama Janelle
Monae, Eminem, Linkin Park, Kanye West, Drake, Usher, Paramore na wengine
wengi.
Jameson wamejipanga kukuza viwango vya burudani kwa
nchi za Afrika Mashariki na awamu hii wamejipanga kwa kuwapa burudani ya pekee
mashabiki watakaohudhuria burudani hiyo huku wakizidi kuwekeza zaidi katika
kuwaleta wasanii wa kimataifa.
Mwaka 2014 Jameson ilifanikiwa kuandaa matamasha mawili makubwa nchini
Kenya ambayo yote tiketi zake zilimalizika kabla huku la kwanza burudani
ikitolewa na wasanii wa ndani, na la pili burudani ilitolewa na msanii 2 Chainz
huku balozi mashuhuri wa Afrika Akon akihudhuria pia.
Akizungumzia kuhusu show
hiyo, Balozi wa Jameson, Antony Owich amesema party ya mwaka huu itazidi kuwa
kubwa na bora kuliko miaka iliyopita.
‘Jameson imejikita katika
kuwapa kumbukumbu za kipekee mashabiki wake na kwa mwaka huu inawaahidi kuwapa
burudani ya pekee kabisa na watu wasikose kuhudhuria’ alisema Owich.