JOSE CHAMELEONE AWAPA SURPRISE YA NGUVU MASHABIKI WA SKYLIGHT BAND, USIKOSE LEO KIOTA CHA ESCAPE ONE
Muimbaji kutoka nchiniUganda Jose Chameleone akiimba kwenye stage ya bendi ya Skylight mara baada ya kupanda kwenye stage hiyo na kuwaacha mashabiki awa bendi hiyo wakitoa shangwe ya nguvu. Njoo leo Skylight imekuandalia suprise za kutosha kutoka katika bendi hii.
Muimbaji wa nchini Uganda Jose Chameleone (katikati) akiimba kwa hisia moja ya nyimbo yake uku akisindikizwa na waimbaji wa bendi ya Skylight kushoto ni Suzy pamoja na Kasongo Junior (kulia).
Sony Masamba ambaye ni mmoja wa waimbaji wa Skylight akiendelea kutoa burudani akisindikizwa na waimbaji wenzake katika kiota cha Escape One Mikocheni.
Waimbaji wa Bendi ya Skylight wakiendelea kutoa burudani ya nguvu kwenye kiota cha Escape One.
Sam Mapenzi ambaye ni mmoja wa waimbaji wa Skylight akitoa burudani ya ngoma za Kinaija huku mashabiki wa bendi hiyo wakiendelea kuzirudi
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiimba sambamba na mashabiki wao nyimbo zinazobamba Afrika ya Mashariki katika hatua yake ya kukusanya mashabiki ili tu waende sawa aisee huyu jamaa ni hatari jumapili hii atakuwepo pale Escape One Mikocheni bila kukosa sogea taratibu uje ushuhudie vitu kutoka Skylight Band.
Kasongo Junior wa Skylight band akiimba na mmoja wa shabiki mkubwa wa bendi ya Skylight jumapili iliyopita katika kiota cha Escape One Mikocheni
Waimbaji wa bendi ya Skylight wakiwafundisha Style mpya ya kucheza wanapokuwa wanacheza nyimbo za bendi hiyo.
Mashabiki wakicheza kwa kuzungusha duala hapa ni kukata mauno mpaka kieleweke.
Binti Royalty_inty_Cakes akikata keki ya kusherekea siku yake ya kuzaliwa uku akiimbiwa nyimbo na Bandi ya Skylight
Hakika Skylight band ni mwisho wa matatizo unaweza kusherekea sikukuu yako kwa kuimbiwa nyimbo na Bendi hiyo
Msanii Em Njenje kutoka bandi ya Wana Njenje naye hakuwa nyuma kuja kuwapa burudani mashabiki wa bamdi ya Skylight ndani ya Kiota cha Escape One Mikocheni.
Waimbaji wa Bandi ya Skylight wakicheza na mashabiki wao katika kiota cha Escape One Mikocheni.
Sam Mapenzi wa Skylight akitoa burudani mbele ya mashabiki wa bendi hiyo katika kiota cha Escape One Mikocheni
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiimba akiimba uku akisindikizwa na wasanii wenzake.
Hakika kwenye shoo ya Skylight ya kila Jumapili sio ya kukosa njoo ujionee mambo mazuri kutoka katika bendi ya Skylight.....Just Follow the Light.