Bukobawadau

KARIBU NEW COFFEE TREE HOTEL BUKOBA

 New Coffee Tree ni hoteli inatoa huduma nzuri ya vyumba vya kulala kwa mtu mmoja mmoja, wawili wawili au zaidi,Vyumba vyake  vinatazama mandhari nzuri ya milima ya Kashura.
New Coffee Tree ni Hotel nzuri yenye usalama wa kutosha wa magari na wateja inapatikana  pembezoni kidogo kama si katikati  mwa mji wa Bukoba, yamata nusu  kilomita kutoka Stend kuu ya mabasi na kilometa moja kutoka Airport  jirani kabisa na Uwanja wa Mpira wa Kaitaba.
New Coffee Tree Hotel  Ipo mahali panapopendeza karibu kabisa na fukwe za ziwa Victoria.
 Ndani ya Ofisi ya Mkurugenzi tunakutana na Bi Rehana Mukadam pichani unaweza kuwasiliana na New Coffee Tree Hotel (Katalyeba Enterprises and General Supplies) kupitia P.O Box 217 Karagwe.
Tel:028 222 1227, Mobile:0743 252668
 Mawasiliano Email:hotelmancoffee@yahoo.com,Website:www.newcoffeetreehotel.com
 Mr. Smart Baitani pichani kushoto akibadilishana mawazo na Mlangira Ben Katruga
Mlangira Ben Kataruga pichani kushoto akibadilishana mawazo na Mzee Bayona pichani kulia


 Mgahawa wa Coffee Tree hotel unaoitwa unatoa huduma ya vyakula mbalimbali, vinavyotolewa ama ndani au nje kwenye eneo la wazi lenye hewa safi na upepo mzuri utokao ziwa Victoria .Huduma katika mgahawa huu ni pamoja na kifungua kinywa, chakula cha mchana na jioni/usiku. Vyakula hivi ni vya mapishi ya Kiafrika, Kihindi, Kichina, Kimataifa,na vinginevyo vya kimataifa ambavyo hutayarishwa na wapishi wataalamu katika jiko lenye vifaa mbalimbali vya kisasa.
Mdau Nellyson akiwa maeneo ya New Coffee Tree Hotel
 Huduma zitolewazo katika eneo lililowazi ni pamoja na huduma za baa kama inavyo onekana pichani
 Wageni mbalimbali wakiendelea kufurahia huduma safi hapo New Coffee Tree Hotel
HUDUMA KWA UJUMLA Baa Gari la kukodi Baa ya kokteli(mchapalo) Huduma za mikutano Kifungua kinywa aina ya kimagharibi Ukumbi wa chakula Udobi, Huduma za Intaneti ,Maegesho salama ya magari, Mgahawa Huduma za vyumbani Vyumba vyenye luninga Huduma ya kuamshwa
Lugha za mawasiliano ni  Kiingereza na Kiswahili
Mpambanaji Muganyizi pichani kushoto na Bwana Kagabo kama walivyo kutwa na Camera yetu
Muonekano wa Chumba ndani ya New Coffee Tree Hotel
 Chumba cha kamili cha kulala bila shaka katika (suti style)
 Burudani ya mchezo wa Pool inahusika bila Kelele ama Vurugu
 Karibu New Coffee Tree Hotel kwa huduma bora, mandhari nzuri bila kuhisi usumbufu!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau