KONGAMANO LA MABADILIKO YA TABIANCHI LAFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO,JIJINI DAR
Mc katika kongaman0 la Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Oxfam Tanzania Suhaila Thawer akiendelea kutoa utaratibu
Eva Mageni ambaye ni Rais wa wakulima wanawake vijijini na alikuwa mshiriki wa shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015, akifungua kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi ambapo alizungumzia kwa kifupi kuhusu mkutano wa COP21 ambao utafanyika Paris Ufaransa hivi karibuni.
Edward Tunyone kutoka Forum CC akieleza maana zaidi ya Mabadiliko ya Tabianchi ambapo alielekeza mazungumzo yake katika majanga asilia, mito kupotea kutokana na shughuli za wanadamu kama kulima jirani na maeneo hayo, mwisho alisisitiza swala la mabadiliko ya Tabianchi ni jukumu la kila mtu na taasisi zinazohusika na mamswala hayo tu.
Bi Mwindiwe makame aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula kutoka Zanzibar, akiendelea kueleza maana ya Mabadiliko ya Tabianchi alisisitiza kutunza mazingira.
Denis Allan kutoka Norwegian Church Aid Actalliance akielezea umuhimu wa kutunza miti.
Kikundi cha Ngonjela wakiendelea Kuburudisha
Kushoto ni Mtaalam wa Mitandao ya kijamii toka Forum CC akitoa maelekezo ya shindano la Instagram
Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza
Aliyewahi kuwa Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2012 St.Matha akielezea jambo kuhusiana na mabadiliko ya Tabianchi
Bw. Gambaedya P.M kutoka Tume ya Ardhi akitoa somo juu ya kilimo hifadhi
Bi.Tatu Kayumbu kutoka Wizara ya Kilimo akieleza ushirikiano wa kilimo na utunzaji wa Mazingira
Kundi la Youth can wakiendelea kutumbuiza
Meneja wa Kampeni Haki ya Uchumi kutoka Oxfam Eluka Kibona akitoa mwongozo wa kikao
Mkutano wa Forum CC ukiendelea
Baadhi ya washiriki wakijadili Michoro ambayo walipewa kazi ya kuipitia na kuijadili.
Kushoto ni Mkurugenzi mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akijumuika na wananchi wengine katika Kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi
Baadhi ya waliokuwa washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula kwa nyakati tofauti wakionesha bidhaa zao
Kushoto ni mmoja wa washiriki waliohudhulia kongamano la mabadiliko ya Tabianchi akipokea zawadi ya tsh 100,000 aliyoshinda Steven Albert.
Baadhi ya washiriki katika Kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi
*******
ASASI za Kiraia nchini zikiwemo Oxfam Tanzania, Forum CC na Norwegian Church Aid Actalliance zafanya kongamano la Kukabiliana na
mabadiliko ya Tabianchi kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa Chakula
nchini.
Akizungumza Afisa Miradi Msaidizi wa
Shirika la Forum CC,Jonathan Sawaya alisema asasi hizo zimeona ni vema
kuwakilisha sauti za wakulima kwa serikali katika kuhakikisha hatua
stahiki zinachukuliwa katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
Alisema asilimia kubwa ya wakulima wengi hasa wanawake
ambao karibia asilimia 70 wamekuwa wakiathirika na Mabadiliko hayo
wakati wanapolima.
Sawaya alisema wananchi wanapaswa kuhifadhi mazingira na
kutunza vyanzo mbalimbali vya maji ili kupunguza athari zitokanazo na
mabadiliko ya tabia nchi.
"Kwa kushirikiana na shirika la Oxfam pamoja na Norwegian
Church Aid tumeamua kufanya kongamano hili ili kupaza sauti za wakulima
na wafugaji katika suala zima la kukabiliana na mabadiliko ya tabia
nchi na serikali kutilia mkazo katika kusimamia suala hili kwa kuongeza
bajeti,"alisema Sawaya
Aidha alisema asilimia kubwa ya wanawake wameonyesha juhudi
mbalimbali za kukabiliana na athari hizo kutokana na wao kujihusisha
katika uzalishaji wa chakula.
"Tuwaunge mkono wazalishaji wa chakula wadogo,wafugaji
pamoja na wavuvi katika suala hili kwa kuwaunganisha na masoko na
kuwapa mikopo,"alisema
Aidha Kongamano hili limehusisha wadau mbalimbali wakiwemo
watendaji wa serikalini,wakulima pamoja na wafugaji katika kuhakikisha
mabadiliko ya tabia nchi yanatokomezwa.
"Kongamano hili ni sehemu ya maandalizi ya Mkuu wa 21 wa
Mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi unaotarajia
kufanyika Novemba 30 nchini Ufaransa,"alisema Sewaya