HAPA NA PALE NA CAMERA YETU DEC 24,2015
Camera yetu mtaani leo Alhamis Dec 24,2015 inakutana na wadau waishio Jijini Dar,kutoka kushoto ni Bwana Tbs, Mr Ben Mulokozi aka Mr.appetizer (Binuzi) na Ndugu Ruta Rwabigene wakiwa tayari kwa ajili ya kusherehekea sikukuu za Krismas na Mwaka mpya nyumbani
Taswira mjini kati
Wadau kama walivyokutwa na Camera yetu wakibadilishana mawazo, hapa na maeneo ya Mtk kwa Dada Jane ajenda kubwa ni lile tamasha lililoandaliwa na Mbunge maarufu kama tamasha la BUMUDECO ambalo litakuwa Jukwaa la kila mwaka la kuwakutanisha wadau wote wenye maslahi na kiu ya dhati ya kuiona Bukoba ikipiga hatua za kimaendeleo kwa kasi inayostahili
Mtaalam mwemezi kimasha pic kushoto akiwa tayari mjini hapa kwa ajili ya kushiriki lile tamasha la Bumudeco
Hekaheka za hapa na pale mbele ya lango la Soko kuu Mjini Bukoba
Bwana TBC akiteta jambo na Dada Jane wa MTK Miembeni
Kutoka Jijijini Dar pichani ni ndugu wa familia ya Marehemu mzee Kahwa,muda mchache kabla ya kuelekea Kijijini Kanyigo kwa ajili ya kusherehekea siku kuu ya
Mdau Ruta Rwabigene katika Ubora wake.
Mdau mpambanaji Bushira mbele ya Camera yetu.
Taswira mjini kati
Wadau kama walivyokutwa na Camera yetu wakibadilishana mawazo, hapa na maeneo ya Mtk kwa Dada Jane ajenda kubwa ni lile tamasha lililoandaliwa na Mbunge maarufu kama tamasha la BUMUDECO ambalo litakuwa Jukwaa la kila mwaka la kuwakutanisha wadau wote wenye maslahi na kiu ya dhati ya kuiona Bukoba ikipiga hatua za kimaendeleo kwa kasi inayostahili
Mtaalam mwemezi kimasha pic kushoto akiwa tayari mjini hapa kwa ajili ya kushiriki lile tamasha la Bumudeco
Hekaheka za hapa na pale mbele ya lango la Soko kuu Mjini Bukoba
Bwana TBC akiteta jambo na Dada Jane wa MTK Miembeni
Kutoka Jijijini Dar pichani ni ndugu wa familia ya Marehemu mzee Kahwa,muda mchache kabla ya kuelekea Kijijini Kanyigo kwa ajili ya kusherehekea siku kuu ya
Mdau Ruta Rwabigene katika Ubora wake.
Mdau mpambanaji Bushira mbele ya Camera yetu.
MWALIKO WA KUSHIRIKI MKUTANO WA
KIMAENDELEO—MANISPAA YA BUKOBA
JUMAPILI, TAREHE 27/12/2015 KUANZIA SAA
10:30 JIONI KATIKA UKUMBI WA ST. THEREZA
1.
UTANGULIZI
Mbuge wa Bukoba Mjini akishirikiana
na Balaza la Madiwani na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba wanapenda
kuwakaribisha wale wote wenye maslahi na maendeleo ya Manispaa ya Bukoba;
ambayo ni sebule ya mkoa wa Kagera, kwenye Kongamano la Kimaendeleo
litakalofahamika kama BUKOBA MUNICIPAL DEVELOPMENTAL CONFERENCE (BUMUDECO). Kongamano hili litafanyika
Jumapili, Tarehe 27/12/2015 kuanzia Saa 10:30 Jioni Mjini Bukoba katika ukumbi
wa St. Theresa. Mpaka sasa watu wa nafasi mbalimbali kutoka ndani na
nje ya Kagera, nchi jirani na nchi za mbali wameonyesha nia ya kutumia likizo
zao za mwisho wa mwaka kushiriki nasi Mkutano huu.
BUMUDECO litakuwa Jukwaa la kila
mwaka la kuwakutanisha wadau wote wenye maslahi na kiu ya dhati ya kuiona
Bukoba ikipiga hatua za kimaendeleo kwa kasi inayostahili. Katika mkutano wake
wa kwanza BUMUDECO inapanga kuwa na shughuli zifuatazo:
·
Kuwasilisha
Mpango-Kazi wa Mbunge na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa
Bukoba kwa kipindi cha mwaka 2015-2020 ikiwa ni tafsiri ya yale walioahidi
katika kipindi cha kuomba kura.
·
Kubainisha
fursa za kibiashara, uchumi na maendeleo zinazopatikana ndani ya Manispaa na
vivutio vitakavyotolewa na uongozi mpya kuvutia na kuhamasisha uwekezaji.
·
Kuthibitisha utayari wa uongozi mpya wa
kisiasa na watendaji wa Manispaa katika kushirikiana na wadau kuondoa mkwamo wa
kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi kubwa
·
Kupokea
mada na Michango mahususi kutoka kwa wanataaluma, wawekezaji na wajasiriamali
mbalimbali kwa ajili ya kupeana ufahamu na uzoefu.
·
Kuanzisha
na kujenga Jukwaa la wadau wa Maendeleo ya Manispaa ya Bukoba kwa ajili ya
kujenga mshikamano wa pamoja, kufahamiana na kuweka utaratibu wa kukutana walau
mara moja kila mwaka.
·
Kutoa
fursa kwa wadau wa ndani na nje ya Bukoba kufurahi pamoja, kuburudika na
kusherehekea mafanikio walioyapata katika shughuli zao kwa mwaka 2015
Pamoja na mwaliko huu, BUMUDECO
inakaribisha wadau kuonyesha nia
(Expression of Interest) katika kuanzisha na kutekeleza miradi
mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kimaendeleo ndani ya Manispaa ya Bukoba.
2.
SEHEMU KUU ZA BUMUDECO 2015
2.1
MKUTANO
Hii
itakuwa sehemu ya kwanza ya tukio la BUMUDECO itakayoanza saa11:00 Jioni na kuhitimishwa saa
2:00 usiku. Katika sehemu hii wageni waalikwa na viongozi nbalimbali
watambulishwa na kutoa salamu. Shughuli kuu katika sehemu hii itakuwa
uwasilishaji wa mada mbalimbali zilizoandaliwa na Wataalam pamoja na
wawakilishi wa makundi ya Jamii. Washiriki wa ndani na nje ya ukumbi watapata
fursa kuchangia mijadala na kila mada itatamatishwa kwa maazimio
yatakayotekelezwa. Taratibu zinafanyika ili kwa kutumia TEHAMA, wadau watakaoshindwa
kushiriki moja kwa moja ukumbini waweze kushiriki kupitia matukio yatakayo
rushwa moja kwa moja kupitia Mtandao.
Mada
na watoa mada watakaowasirisha mada ni hawa wafuataio:
S/No.
|
Mtoa Mada
|
Mada
|
1
|
Leopard
Rweyemamu
|
Fursa
za Uwekezaji na Utayari wa Manispaa ya Bukoba Kufanikisha Miradi ya Maendeleo
|
2
|
Ali
Mufuruki
|
Umuhimu
wa Taasisi za Kifedha na Jitihada za Wadau wa Kagera
|
3
|
Anic
Kashasha
|
Ushawishi
kwa Wawekezaji na Hatua za Mafanikio—Mtazamo
wa Sekta Binafsi
|
4
|
Prof.
Lwaitama
|
Historia
ya Mafanikio ya Elimu Mkoani Kagera; Tunarejeaje Kileleni?
|
5
|
William
O. Rutta
|
Nafasi
ya Utalii katika Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera; Fursa na Changamoto
|
6
|
Jamal
Malinzi
|
Michezo
kama Uwekezaji na Ajira; Nini Fursa za Kagera?
|
7
|
John
G. Ndibalema
|
Mchango
wa Vijana katika Kagera ya Leo na Kesho
|
2.2
SHEREHE
Baada
ya saa 2:30 usiku, mara tu baada ya mkutano kufungwa, mpangilio wa ukumbi
utabadilishwa na maeneo ya wazi katika viwanja vya St. Thereza vitatumika kwa sehemu
ya pili ya tukio la BUMUDECO ambayo itakuwa Sherehe yenye maudhui ya
kufahamiana na kupongezana kwa yote ambayo Mungu amejalia kuyafanikisha katika
mwaka wa 2015. Washiriki watapewa nafasi ya kuchanganyika, kuzungumza,
kubadilisha mawasiliano huku wakipata burudani, vinywaji na chakula. Kwa
kiwango cha kutosha viburudisho katika sherehe hii vitalenga kudhihirisha
utajiri wa tamaduni za Mhaya lakini pasipo kuwapunja wale wanaopenda radha
tofauti.
3.
KUSHIRIKI
Mpaka
dakika hii, Kamati imefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha malengo ya
BUMUDECO 2015 yanatimia na kila mdau anaridhika kwa muda na rasilimali zake
atakazozitenga ili kushiriki tukio hili. Kwa kuzingatia matarajio, maoni na
mapendekezo ya wadau, Kamati imeridhia pendekezo la TZS 50,000/= (Elfu hamsini)
kama ada ya uanachama wa kujiunga na BUMUDECO. Kwa ada hii, pamoja na
kutambulika rasmi kama mwanachama kwa mwaka mzima, mdau atapata tiketi ya
kushiriki mkutano wa BUMUDECO 2015, atahudhuria sherehe na atapewa huduma zote
za vinywaji, chakula na burudani. Pia wadau wote watakaoshiriki BUMUDECO 2015
wataingizwa kwenye kanzidata yakupewa Taarifa za Mkutano na maendeleo ya
utekelezaji wa maazimio ya mkutano.
3.1
JINSI YA KULIPIA NA KUPATA KADI
Kadi
zinapatikana Bukoba Mjini katika vituo vifuatavyo:
·
Uswahili Manyema
Café
·
Total Petrol
Station
·
Ofisi ya Meya wa
Manispaa
·
Ofisi ya Mbunge
Bukoba
·
Ofisi ya
Mkurugenzi
Pia
Kamati imesajili namba maalumu za mitandao mitatu kumsaidia mshiriki kutuma ada
yake. Kupata tiketi yako tuma TZS 50,000/= kwenye moja ya namba zifuatazo:
·
M-Pesa
0743-059-595;
·
Airtel Money 0785-311-884;
·
tiGo-Pesa
0717-656-769
NAMBA
ZOTE ZINASOMEKA JINA: BUMUDECO BUKOBA. Pesa yako itakapopokelewa utapigiwa simu
na Mwanakamati atakayechukua majina yako kamili na kukupatia neno-siri/nywila
utakayotumia kuingia kushiriki BUMUDECO 2015.
KARIBU
NYOTE/MUNYEGERE WAITU!
Imetolewa na Kamati ya Maandalizi