KAGERA WAASWA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI ILI KUKUZA UCHUMI WA MKOA NA TAIFA KUPITA SEKTA ZA VIWANDA BIASHARA NA UWEKEZAJI
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Charles Mwijage asistiza kumalizwa kwa migogoro ya ardhi kwa
maridhiano bila kupelekana mahakamani kati ya wananchi na wawekezaji ili kukuza
sekta za viwanda na biashara na kuinua uchumi wa mkoa wa Kagera wenye fursa nyingi za uwekezaji hasa katika sekta za viwanda na biasahara.
Waziri Mwijage aliyasema hayo katika
majumuisho ya ziara yake ya siku mbili mkoani Kagera aliyoifanya tarehe 04 hadi
05.01.2016 ambapo alitembelea viwanda
vya Vickfish,TANICA, Hamir Hamza Tanzania Ltd vilivyopo katika Manispaa ya
Bukoba. Vilevile Waziri Mwijage alivitembelea viwanda vya Kagera Tea Company
Ltd, Kagera Fish katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya
Muleba alitembelea shamba la chai la Binengo Izigo na alimalizia ziara yake
katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kwa kutembelea kiwanda cha Kagera
Sukari na eneo lilotengwa kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya viwanda
(Export Processing Zone, EPZ) lililopo Omukajunguti lenye hekta 3000.
Dhumuni la kutembelea viwanda
hivyo Waziri Mwijage lisema ni kuhakikisha vinafanya kazi ipasavyo kwa kiwango
serikali ilichokusudia na kuhakikisha asilimia 40% ya Watanzania ambao ni nguvu
kazi wanafanya kazi katika viwanda na kuzalisha kwa wingi ili viwanda hivyo
viweze kuchangia katika pato la taifa kwa asilimia 15% ifikapo mwaka 2020
Kuhakikisha Watanzania waliopo
katika sekta ya viwanda wanafanya kazi wanazotakiwa kuzifanya kwa kujifunza
teknolojia mpya badala ya kuendelea kuwategemea wataalam kutoka nje tu. Viwanda
kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi kwa kuhakikisha waajiliwa wanapewa stahiki na haki
zao bila migogoro yoyote ile wawapo kazini.
Kuhakikisha Watanzania waliopo
katika sekta ya viwanda wanafanya kazi wanazotakiwa kuzifanya kwa kujifunza
teknolojia mpya badala ya kuendelea kuwategemea wataalam kutoka nje tu. Viwanda
kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi kwa kuhakikisha waajiliwa wanapewa stahiki na haki
zao bila migogoro yoyote ile wawapo kazini.
Waziri Mwijage kwa kutoa wigo mpana katika sekta ya uwekezaji hasa viwanda aliagiza kila Halmashauri nchini
kuhakikisha zinatenga maeneo ya kujenga
au kuanzisha mitaa ya SIDO ili kutoa
fursa kwa wajasiliamali wadogowadogo kufanya shughuli zao katika eneo moja lilotengwa na kujengwa au
kugawanywa kitaalamu na wataalam kutoka katika Wizara yake ambao wako tayari
kufanya kazi hiyo.
Nao wadau wa uwekezaji hasa wafugaji wanaofuga
kisasa waliohudhulia kikao cha
majumuisho cha Waziri Mwijage waliiomba serikali kuangalia uwezekano wa
kuwamilikisha ardhi au vitalu wanavyovimiliki kwa kuwapatia hati kamili badala
ya kupangishwa na NARCO ili waweze kukopa na kuendeleza ufugaji wa kisasa
zaidi, aidha serikali kuwa inatoa majibu kwa wakati na haraka kwenye masuala ya
kukuza uchumi wa nchi.