MKUTANO MKUU WA KADEA JAN 5,2016
Meza kuu wakiongozwa kuimba wimbo maalum wa KADE(ndi wa KADEA akala na kalenge)
Viongozi wakuu wa KADEA
Mwenyekiti,Enock Kamuzora akiwasilisha taarifa yake kwa wajumbe wa mkutano mkuu
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo mkuu
Viongozi wakuu wa KADEA
Mwenyekiti,Enock Kamuzora akiwasilisha taarifa yake kwa wajumbe wa mkutano mkuu
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo mkuu
MKUTANO mkuu
wa shirika la maendeleo ya wananchi wa Kata za Kanyigo na Kashenye-KADEA kwa mwaka 2015,umefanyika 05 Januari mwaka
huu,pamoja na mambo mengine ,umeazimia kuendelea kuchangia mfuko wake wa elimu
kwa ajili ya kuinua elimu katika shule za msingi kwa kata hizo mbili.
Mfuko huo wa
elimu ulioanzishwa mwaka 2012 umesaidia kupandisha kiwango cha ufaulu kutoka
wanafunzi 400 hadi zaidi ya wanafunzi 400 wanaojiunga na sekondari sasa.
Mwenyekiti
wa KADEA,Enock Kamuzora,akiwasilisha ripoti yake kwa wajumbe wa mkutano
mkuu,alisema mwaka 2015 Mei, mtihani wa mock wa Mkoa wa Kagera kwa darasa la
saba,kwa kata ishirini za Wilaya ya Missenyi,Kata Kanyigo ilishika nafasi ya
kwanza na Kashenye nafasi ya pili.
Katika
mtihani wa Taifa wa darasa la saba wa mwezi Septemba mwaka jana,Wilaya ya
Missenyi,Kata Kanyigo ilikuwa ya kwanza na Kashenye ya tatu.
Aidha kwa
miaka mitatu mfululizo,katika shule ya sekondari Kanyigo,inayomilikiwa na
shirika hilo,hakuna mwanafuzi yeyote aliyefeli katika mitihani ya Taifa ya
kidato cha pili,nne na sita.