Bukobawadau

MWILI WA MAREHEMU PROF. LADISLAUS LWAMBUKA WAAGWA NYUMBANI KWAKE MBEZI BEACH JIJINI DAR ES SALAAM

 Jana jioni ilifanyika misa ya kumwombea na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Prof. Ladislaus Rwambuka aliyefariki juzi jumapili katika hospitali ya Kairuki ya Mikocheni. Misa hii imefanyika nyumbani kwake eneo la Mbezi Beach. 
 Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa leo kuanzia saa mbili za asubuhi katika ukumbi wa Nkuruma katika chuo kikuu cha Dar es salaam na kufatiwa na safari ya kuelekea Bukoba kwa ajili ya mazishi yatakayo fanyika nyumbani kwake Kijijini  Ishozi -Katano.
 Ibada ya kumuombea Marehemumarehemu Prof. Ladislaus Lwambuka ikiendelea,marehemu  Kabla ya kufikwa na umauti alikuwa ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam. Picha zote na team ya Pamoja Blog.
 Mchumgaji Mpesha Lwambuka ambaye ni kaka yake na Marehemu kutoka Marekani akitoa mafundisho kwa ndugu na jamaa waliofika nyumbani kwa marehemu wakati wa misa ya kumwombea marehemu Prof. Ladislaus Rwambuka 
 Mchumgaji Mpesha Rwambuka akimwombea mke wa marehemu wakati wa misa ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyka nyumbani kwake Mbezi Beach.
  Mchumgaji Mpesha Rwambuka akimwombea mtoto wa mwisho kwa niaba ya watoto wote wa marehemu 
Ndugu na jamaa wakiendelea kusikiliza mafundisho kutoka kwa mchungaji

Bw. Ezlael Kamzora ambaye ni mdogo wake marehemu akisema jambo pamoja na kuwatambulisha mke pamoja na watoto wa marehemu kwa ndugu, jamaa na marafiki waliofika katika misa ya kumwombea marehemu Prof. Ladislaus Rwambuka iliyofanyika nyumbani kwake Mbezi Beach.

Mke wa marehemu Bi Josephine akiwa amesimama wakati wa kutambulishwa kwa baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika nyumbani kwa marehemu.

Baadhi ya watoto wa marehemu wakati wakitambulishwa 

 Baadhi ya marafiki wa karibu wa marehemu wakiwa kwenye misa ya kumwombea rafiki yao kipenzi marehemu Prof. Ladislaus Lwambuka.

Mwenyekiti wa Lugoye, Prof. Kahamba(kushoto) akizungumza  jambo mbele ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika kwenye misa ya kumwombea marehemu Prof. Ladislaus Lwambuka aliyefafiki siku ya jumapili na kulia ni mweka azina Bw. Bushoke.
 Mwakilishi wa Tawi la Yanga Tabata Kisiwani ambapo Prof. Lwambuka alikuwa mlezi wao  akizungumza jambo kuhusu marehemu na kutoa salamu za pole kwa ndugu na jamaa kwa msiba mkubwa uliowakuta.
 Mwakilishi wa Mbunge wa Kawe akizungumza jambo wakati wa misa ya kumwombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Mbezi Beach
Baadhi ya wanachama wa Lugoye wakifuatilia matukio yanayoendelea,kutoka kushoto pichani ni Mzee Gosbart Matambula,Adv.Erasmus Buberwa,Mlangira Ben Kataruga na Bw.Charles Mbelwa
Mdogo wa Marehemu akiongoza nyimbo wakati wa misa ya kuaga mwili wa kaka yake nyumbani kwake Mbezi Beach.


 Baadhi ya ndugu jamaa na marakifi waliofika nyumbani kwa marehemu kuuaga mwili wake.
 Mjane wa Marehemu Bi Josephine akiaga kwa uchungu mwili wa mme marehemu Prof. Ladislaus Lwambuka aliyefariki siku ya jumapili katika hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam 
Mtoto wa maremu akilia kwa uchungu wakati wa kuagwa kwa mwili wa baba ye
Watoto wa marehemu wakilia kwa uchungu wakati wa kuaga mwili wa baba yao
Mzee Mhandiki ambaye ni mmoja wa wanafamilia akitoa heshima kwenye mwili wa marehemu.
 Mwenyekiti wa Lugoye, Prof. Kahamba(wa kwanza kulia) akitoa heshima zake za mwisho kwenye mwili wa marehemu na wa pili kuytoka kulia ni Focus Lutinwa
 Mzee Josian Mnazi(wa kwanza kulia) akiaga mwili wa marehemu
 Mzee Erasmus  Machume wakati akiaga mwili wa marehemu
Bw. Mutabuzi akiaga mwili wa marehemu
 Bw. Charles Mbelwa mwanachama wa Lugoye akiaga mwili wa maremu
 Mzee Gosbart Matambula akitoa heshima zake za mwisho
 Adv.Erasmus  Buberwa akiaga mwili wa marehemu
 Mzee Kiiza(mwenye sharti nyeupe) akiaga mwili wa marehemu
 Mlangira Ben Kataruga(mwenye suti nyeusi) akiaga mwili wa marehemu
Katikati ni Mzee Kiiza aliyekuwa  mwenyekiti wa zamani wa Kikundi cha Lugoye
Anaonekana Mlangira Ben Kataruga akitoa heshima zake kwa Mwili wa Marehemu Prof Lwambuka

 Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakiaga mwili wa marehemu Prof. Ladislaus Lwambuka.
BUKOBAWADAU MEDIA tunatoa pole kwa familia yake na wanachama wa 'Lugoye Social Club' Tunamuomba Mwenyezi Mungu aipokee roho ya marehemu Milele AMEEN!
TUJIKUMBUSHE :Marehemu Prof Ladislaus Lwambuka (kushoto) wakati wa Uhai wake, hii ilikuwa katika hafla ya mwaka ya Kikundi cha'Lugoye Social Club'
 iliyofanyika tarehe 27 Dec 2015 mwezi mmoja uliopita nyumbani kwa  Mzee Josian MunaziKijijini Gera Kashekya
Dec 27,2015 Marehemu Prof Ladislaus Lwambuka wa pili kushoto enzi za uhai wake katika picha na baadhi ya wanachama wa Kikundi 'Lugoye Social Club'

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe....Ameen.!! 

Next Post Previous Post
Bukobawadau