Bukobawadau

KOO ZA BUHAYA, TAMADUNI NA MIIKO

Koo, tamaduni na miiko katika Buhaya ni vitu ambavyo vinatambulika na vina maana sana katika kumwelezea mtu husika katika mambo mbali mbali ya kijamii katika Buhaya.
Mambo haya yameanza kupotea, mbaya zaidi vijana wengi hawajapata fursa ya kufahamu haya mambo na wengine kushindwa kabisa hata kufahamu koo zao kutokana na sababu mbali mbali.
BUKOBAWADAU MEDIA inatumia jukwaa lake kuangazia mambo mbali mbali ya koo ili kuwapa mwanya vijana kufahamu kwa kina mambo haya.

Kwa kuanza; kika mtu ataje ukoo wake ili tujue ni koo ipi inawatu wengi zaidi na Tutakua tukijadili ukoo mmoja mmoja, na ukoo wenye watu wengi zaidi ndio tutaanza nao
Inasemekana kuwa wahaya walitokea Misri na kupitia Uganda na hatimaye kuanza maisha katika eneo la Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania
Wakati wamishenari wa Ulaya walipowasili, eneo hilo lilikuwa maarufu kwa kuwa na Kadinali wa kwanza wa kikatoliki marehemu Laurian Rugambwa.

Aidha watu wa Jamii hii walizingatia sana elimu ikilinganishwa na makabila mengine nchini Tanzania
Kabla ya kuwa na serikali ya taifa watemi ndio walitambuliwa kama wakuu wa jamii ya Wahaya.
Ndoa ni swala linaloheshimiwa katika kila jamii, na ni jambo linaloenziwa sana na jamii ya Wahaya.
Mahari ya Ng'ombe ama mbuzi ilitolewa kwa baba wa msichana kulingana na makubaliano ya pande zote mbili.
Wahaya wana koo 8 ambazo ni Bumbira, Edangabo, Ganda-Kiaka, Hamba, Hangiro, Mwani, Nyakisisa, Ekiziba na Yoza.

Ni wazi kuwa jamii ya wahaya ni watu waliojitambua mapema.Sifa na utamaduni wetu ni muhimu kuvitunza kwa manufaa ya sasa na baadae.Kushindwa kuenzi vitu hivyo ,vizazi vijavyo vitakuwa watumwa wa jamii na tamaduni nyingine.
Hivyo mdau msomaji toa maoni yako tueleze unatoka Ukoo gani (Oluganda )sifa za ukoo huo na miiko yake na chochote unachokijua kuhusu ukoo fulani..

Kumbuka ku like na kushare ukurasa wetu wa Bukobawadau Entertainment Media
Next Post Previous Post
Bukobawadau