Bukobawadau

MAONI KUTOKA KWA MDAU WETU

Habari za usiku wapendwa Watanzania wenzangu.
Leo nataka niongelee suala ambalo ni sensitive kidogo, na sio kidogo ni sensitive sana kwa sababu linahusu usalama wetu, kwa lugha za wenzetu wanasema SAFETY kwenye vivuko vyetu vya Kigamboni. Mimi ni mtumiaji mkubwa wa vivuko vya Kigamboni, hiki kidogo na kile kikubwa, kwa wiki naweza kuvuka kwenda Kigamboni zaidi ya mara 3. Kwa hiyo ninachokiandika hapa kinatokana na yale niliyoyaona na ninayoendelea kuyaona hapo Kivukoni, tunasema through observation, au participatory observation. Nitafocus kwenye kipengele cha usalama/safety tu, ingawa kuna mambo mengi yanayojiri katika eneo hilo, hayo nitayaweka kapuni nitayazungumzia siku nyingine.
Kiukweli hali ya usalama/safety (acha niache hili neno nilitaje kwa kizungu ili kupata maana ninayokusudia kwa sababu neno usalama ni pana zaidi na lina maana zaidi ya moja) kwenye vivuko vyetu inazidi kupungua siku hadi siku. Leo nitaongelea jambo moja tu ambalo linanitia hofu kubwa nalo ni msongamano wa watu ndani ya kivuko kidogo. Huwa ninajiuliza kila mara ninapopanda kwenye hicho kivuko je kuna idadi maalum ya watu wanaoruhusiwa kupanda humo? Je hakuna ukomo wa watu kupanda kwenye hicho kivuko? Na je kama ikitokea dharura yoyote ile baharini kuna idadi ya kutosha ya vifaa vya uokoaji kwenye hivyo viivuko vyote viwili?
 Maswali yangu na wasiwasi wangu yanatokana na hali halisi inayoendelea hapo Kivukoni. Kuna siku mida ya saa 5 asubuhi kulikuwa na watu wengi sana upande wa Ferry/Kivukoni na vivuko vyote viwili vilikuwa upande wa Kigamboni. Kivuko kikubwa kikatangulia kufika Ferry, magari na watu waliomo wakataremka, magari mengine yakaingia ndani ya kivuko, wakati magari yanapakiwa kikaja kivuko kidogo na geti likafunguliwa watu wote tukaambiwa tuingie ndani ya kivuko kidogo ambacho hakikupakia magari. Watu walikuwa wengi sana, mpaka wakajaa ndani ya kivuko kidogo.
Mimi na watu wengine tukaamua kutoingia ndani ya hicho kivuko kwa kuhofia safety yetu. Kulikuwa na askari polisi ambaye alikuwa anahimiza watu wote tukapande kwenye kivuko kidogo ambacho kilikuwa kimejaa kupita kiasi huku anazuia watu kuingia kwenye kivuko kikubwa ambacho kina sehemu ya kutosha kukaa watu juu. Nikamuuliza askari yule aliyekuwa anatuzuia kuwa haoni kama kivuko kidogo kimejaa watu wengi na ikitokea dharura je? Bado akagoma akatuambia hicho kivuko kikubwa hatupandi na kama hatutaki kupanda hicho kilichojaa basi tukae hapo hapo tusubiri mpaka safari nyingine. Kufupisha story sisi tukaendelea na msimamo wetu kugomea kupanda, na wale waliopanda mule wakawa wanapangwa kama askari walioko kwenye paredi ili watoshe mle ndani na waondoke kwenye mlango wa kivuko walikokaa.
Vivuko vyote vikaondoka, kidogo kikiwa kimejaa abiria na kikubwa kikiwa kimebeba magari tu na juu hakuna watu. Bahati nzuri vivuko vile vikarudishwa nyuma vikiwa vimeshaanza safari kupisha meli iliyokuwa inatoka bandarini (sijui hakuna mawasiliano kati ya control tower na manahodha wa vivuko???) ikawa hakuna jinsi tukaruhusiwa kuingia kwenye kivuko kikubwa na watu wengine wakatumia common sense wakahama kutoka kivuko kidogo kuhamia kikubwa. Hilo ni tukio lilitokea siku 1 kabla ya hilo tukio mnaloliona kwenye picha. MwenyeziMungu anasema jisaidie nikusaidie, ifike mahali sisi wenyewe watumiaji na wanaohusika na kuvusha watu tufuate kanuni ya SAFETY FIRST, tuweke mbele usalama wa watu kwanza ili kuepuka majanga ambayo yanaweza kuepukika.
Alamsiki!
Next Post Previous Post
Bukobawadau