Bukobawadau

MAWAZIRI WA ZAMANI MRAMBA, YONA WAENDELEA KUTUMIKIA ADHABU YA USAFI WA MAZINGIRA HOSPITALI YA PALESTINA SINZA JIJINI DAR ES SALAAM

 Waziri wa Fedha wa zamani, Basil Pesambili Mramba (kushoto), akijipangusa jasho wakati akienda kusaini fomu kwa Ofisa Afya Mazingira wa Hospitali ya Serikali ya Sinza Palestina, Miriam  Mong (kulia), baada ya kufanya usafi katika maeneo kadhaa ya hospitali hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, ikiwa ni adhabu ya kutumikia kifungo cha nje hadi Novemba 5 mwaka huu.

Mawaziri wa Fedha wa zamani, Basil Mramba (kushoto) na Daniel Yona wakienda kusaini fomu kwa Ofisa Afya Mazingira wa Hospitali ya Serikali ya Sinza Palestina, Miriam  Mong baada ya kufanya usafi katika maeneo kadhaa ya hospitali hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, ikiwa ni adhabu ya kutumikia kifungo cha nje hadi Novemba 5 mwaka huu.

Na Dotto Mwaibale

ALIYEKUWA Waziri wa Fedha, Basil Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona wanaendelea kutumikia kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika Hospitali ya Sinza Palestina.

Yona na Mramba wanaendelea na hatua hiyo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisuu kuridhia kutumikia kifungo hicho baada ya Magereza kuwasilisha orodha ya majina ya wafungwa ambapo wao ni miongoni mwa watu ambao walionekana kuweza kutumikia kifungo hicho cha nje  kitakachoisha Novemba 5 mwaka.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi, Ofisa Afya Mazingira wa Hospitali hiyo Miriam Mong ambaye pia anawasimamia alisema wamekuwa wakionesha ushirikiano katika kutimiza majuku waliyopatiwa.

"Wanaanza saa mbili asubuhi hadi saa nne, lakini wamekuwa wakionesha ushirikiano kila wanapofika katika kutimiza majukumu yao," alisema.

Alisema leo walifanya usafi katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya kupigadeki katika makorido ya wodi ya wazazi na maeneo ya nje na kesho watafanya katika wodi ambayo wanatibiwa wagonjwa wa kuja na kuondoka OPD na wanafanya usafi kwa awamu," alisema.

Alisema endapo ikitokea wakafanya usafi katika eneo fulani ambalo halikung'aa  watalazimika kurudia.



Next Post Previous Post
Bukobawadau