Bukobawadau

BALOZI DR DIODORUS KAMALA ACHANGIA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA KATA YA KITOBO


Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (pichani) akiongea na wananchi wa Kata ya Kitobo jimboni humo katika mkutano wake na wananchi uliofanyika Jana Feb 29,2016 katika shule ya Msingi Mbale,Balozi Kamala alichangia miradi mbalimbali ya maendelewa katika kata hiyo ikiwa ni pamoja na kuchangia mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Chumba cha maabara katika Shule ya Sekondari ya Bwabuki na kuahidi mifuko 20 ya Saruji kwa ajili ya Ukarabati wa Ujenzi wa Shule ya msingi Kyazi.
Mzee Kabandwa mkazi wa Kijiji cha Kyakakombo kata Kitobo akihuliza swala.
Kabla ya kuongea na Wananchi wa Kitoba, Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala Mbunge wa Jimbo la Nkenge amepokea taarifa ya maendeleo ya kata hiyo yenye Vijiji 5 vya ambavyo ni Kyazi,Kitobo,Mbale,Kashasha na Kijunga vyenye jumla ya Vitongoji 17 na Kaya 1718 zenye wakazi 7437 kati yao wanaume ni 3450 na wanawake ni 3987 wenye uwezo wa kufanya kazi
Bwana Nelson akieleza Kero yake kwa Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala Mbunge wa Jimbo la Nkenge
Bango la Shule ya Msingi Mbale-Kitobo
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbale akifuatilia mkutano huo
Diwani wa Kata ya Kitobo Ndugu Willy Mtayoba akitolea jambo ufafanuzi katika mkutano huo
Mmoja wa Wananchi katika hali ya umakini

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Missenyi Bwana Projetus Tegaamaisho akiongea na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo, Bwana Tegaamaisho ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi wawe na utamaduni wa kuchangia maendeleo ya vijiji vyao
Bwana Wilson B. Kato mtendaji wa Kata Kitobo aitoa taarifa fupi ya maendeleo ya kata hiyo kwa Mh. Mbunge Balozi Dr.Diodorus Kamala ambapo ameanza kwa kumpongeza Mbunge kwa ushindi wa kishindo na kumuelezea matatizo ya huduma za kijamii Elimu,kilimo na mifugo, Afya na Nishati



Makundi ya watu waiendelea kufuatilia kwa kina kinachojiri
Baadhi ya wananchi wakiendelea kumsikiliza mbunge wao Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala
Taswira wakati mkutano ukiendelea

Mlinzi wa Shule ya Msingi Mbale Bw Bonface Mjwahuzi akieleza matatazo binafi yanayomkabili
Wananchi wakiendelea kufuatilia yanayojiri kutoka kwa Viongozi wao

Uongozi wa Kata Kitobo unatoa shukrani kwa Halmashauri ya Wilaya Missenyi kwa matengenezo ya Barabara ya Kyabajwa hadi Kyazi,Mbale,Kashasha hadi Bwanjai ,Barabara hizo zinapitika bila matatizo Wanaiomba Serikali iweze kufanyia ukarabati barabara ya Kyabajwa hadi Kyazi kwa maana  imeanza kuaribika

Uongozi wa Kata Kitobo umetumia fursa hiyo kumshukuru Mh Mbunge Balozi Dr Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala kwa juhudi zake binafsi za kuimiza maendeleo alizokuwa  ameanzisha apo awali Ujenzi wa Daraja la Kabingo umekamilika na kuwaunganisha wananchi na kata jirani ya Bugorora

Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala Mbunge wa Jimbo la Nkenge akipokea zawadi kutoka kwa Vikundi vya Akinana wa Kata Kitobo baada ya kumaliza kuongea nao kuahidi kutatua kero mbalimbali ikiwa ni katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala Mbunge wa Jimbo la Nkenge akifurahi mara baada ya kupokea zawadi kutoka kwa Vikundi vya Akinana wa Kata Kitobo.
Mwisho BUKOBAWADAU MEDIA tunatumia fursa hiikukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241.
Next Post Previous Post
Bukobawadau