BALOZI DR KAMALA AENDELEZA ZIARA KWA KUTEMBELEA VYUO VYA UFUNDI VYA PARTAGE
Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dk. Diodorus Kamala akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Ufundi Byayungu kilichopo Kanyigo-Missenyi Bwana Deusidedith Mwijage pichani kushoto wakati akiwa katika ziara ya kutembelea Vyuo mbalimbali vya Ufundi vilivyomo ndani ya Jimbo lake.
Balozi Dk. Diodorus Kamala kwa kutambua kuwa vijana ndio nguvu kazi ya Wilaya ya Missenyi na Taifa kwa ujumla, ameamua kufanya ziara katika vyuo vya Ufundi ili kuona ni namna gani ataweza kusaidia vijana, hii ni katika kutekeleza Ilani yake mpango mpango wa kupeleka vijana kumi (10) kutoka kila Kijiji kuwapeleka katika Vyuo mbalimbali kwa ajili ya kuwapatia mafunzo maalumu.
Hii inatokana na ukweli kwamba zaidi ya asilimia tisini 90% ya Vijana wanaomaliza kidato cha nne Wilayani Missenyi hawapati nafasi ya kuendelea na elimu ya juu. Mpango huo utasaidia kutengeneza ajira,kukuza kipato,kuandaa mifano (models) kwa vijana wenzao, kupunguza uhalifu, ulevi,vijiwe n.k
St .Dinna Nkondo pichani kushoto wakati akitoa neno la Shukrani kwa Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dk. Diodorus Kamala kutembelea Chuo hicho
Hii inatokana na ukweli kwamba zaidi ya asilimia tisini 90% ya Vijana wanaomaliza kidato cha nne Wilayani Missenyi hawapati nafasi ya kuendelea na elimu ya juu. Mpango huo utasaidia kutengeneza ajira,kukuza kipato,kuandaa mifano (models) kwa vijana wenzao, kupunguza uhalifu, ulevi,vijiwe n.k
Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dk. Diodorus Kamala ametoa wito kwa wananchi wa Missenyi kutowaacha vijana wao waliomaliza Elimu ya Msingi na Kidato cha nne bila msaada na badala yake kuwapeleka vyuo vya ufundi ili waweze kujiajiri.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Bwoki
Balozi Dk. Diodorus Kamala akipata maelezo kutoka kwa Makamu wa Chuo cha Partage cha Bwoki Mwl.Zamda Mohamed alipotembelea Chuo hicho kinachotoa mafunzo mbalimbali
Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimsikiliza kwa makini Mwalimu wa Ufumaji Benitha Johnson pichani kushoto wakati mwanafunzi Lilian Mjongo akiendelea akidalizi.
Balozi Kamala amehaidi kusomesha Vijana
Kumi kutoka kila Kijiji ndani ya Jimbo la Nkenge katika Vyuo mbalimbali
vya Ufundi kwa nia ya kuwawezesha kujiajiri na kuongeza kasi ya
kupambana na umasikini. Jimbo la Nkenge lina vijiji 75.
Mkurugenzi wa Elimu Shirika la Partage, Theodory Kaiyuzi akitolea jambo Ufafanuzi kwa Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dk. Diodorus Kamala wakati wa ziara yake Chuoni hapoSt .Dinna Nkondo pichani kushoto wakati akitoa neno la Shukrani kwa Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dk. Diodorus Kamala kutembelea Chuo hicho
Baadhi ya walimu wa Chuo cha Ufundi cha Partage kilichopo Bwoki Wilayani Missenyi
KWA UJUMLA ZIARA YA MH BALOZI DR. DIODORUS BUBERWA KAMALA JIMBONI NKENGE
Mh Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala alifanya ziara jimboni kwake Nkenge kwaajili ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa kipindi cha miaka mitano, pia kwa kumchagua kwa kura nyingi Mh John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na kuwachagua madiwani wa chama cha mapinduzi. Vile vile Mh Balozi Kamala alitumia fursa hiyo kuongea na wananchi katika kata zote zilizoko jimboni Nkenge ili kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuangalia jinsi ya kuzitatua. Ziara hiyo ilimfikisha Mh Balozi Kamala katika vijiji vyote vilivyoko katika jimbo la Nkenge wilaya ya Missenyi.
Katika zira
hiyo iliyodumu kipindi cha wiki mbili, Mh Balozi Kamala alitembelea
shule mbalimbali jimboni ili kujionea mwenyewe utekelezaji wa Sera ya
Elimu Bure. Mh Balozi Kamala alitumia fursa hiyo kuongea na walimu wa
kuu wa shule za msingi na sekondari kujua changamoto mbalimbali
wanazokumbana nazo katika utekelezaji wa Sera ya Elimu Bure. Matatizo
mbalimbali yaliweza kuibuliwa na walimu hususani uchakavu wa miundo
mbinu mfano vyumba vya madarasa, uhaba wa madawati n.k. Mh. Balozi
Kamala katika kuunga mkono jitihada za Mh Rais Magufuli, Mh mbunge
alichangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika baadhi ya shule jimboni
Nkenge.
Vilevile Mh Balozi Kamala alitembelea vyuo vya ufundi stadi wilayani Missenyi vinavyosimamiwa na shirika la Partage ili kujua jinsi vinavyofanya kazi. Lengo hasa la kutembelea vyuo hivi kwa mujibu wa maelezo ya Mh. Balozi Kamala, ni kuhakikisha anapata vijana kumi kila kata ambao atawasomesha katika vyuo hivi ili baadae waweze kujiajiri wenyewe katika shughuli mbalimbali za ufundi.
Balozi
Kamala pia alichangia michango mbalimbali hususani kwenye sekta ya
michezo ambapo alitoa jezi, mipira na fedha taslimu kwa timu mbalimbali
za kata jimboni Nkenge ili ziweze kushiriki katika mashindano
mbalimbali.
Mh
Balozi Kamala alitumia fursa hii kuwataka wananchi kufanya kazi kiwa
bidii ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya HAPA
KAZI TU. Aliwataka wananchi katika vijiji mbalimbali kutokuendekeza
unywaji pombe uliokithiri hasa nyakati za kazi. Aliwaagiza madiwani wote
kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ilani ya uchaguzi ya chama cha
mapinduzi ili kuondoa umaskini uliokithiri kwa wananchi.
Mwisho Mh Balozi Kamala alitembelea vyuo vya ufundi stadi wilayani Missenyi vinavyosimamiwa na shirika la Partage ili kujua jinsi vinavyofanya kazi. Lengo hasa la kutembelea vyuo hivi kwa mujibu wa maelezo ya Mh. Balozi Kamala, ni kuhakikisha anapata vijana kumi kila kata ambao atawasomesha katika vyuo hivi ili baadae waweze kujiajiri wenyewe katika shughuli mbalimbali za ufundi.
Balozi Kamala pia alichangia michango mbalimbali hususani kwenye sekta ya michezo ambapo alitoa jezi, mipira na fedha taslimu kwa timu mbalimbali za kata jimboni Nkenge ili ziweze kushiriki katika mashindano mbalimbali.
Mh Balozi Kamala alitumia fursa hii kuwataka wananchi kufanya kazi kiwa bidii ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya HAPA KAZI TU. Aliwataka wananchi katika vijiji mbalimbali kutokuendekeza unywaji pombe uliokithiri hasa nyakati za kazi. Aliwaagiza madiwani wote kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ili kuondoa umaskini uliokithiri kwa wananchi.