WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KATIKA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA ATOA RAI MKOA HUO KULINDWA NA WAHAMIAJI HARAMU TOKA NCHI JIRANI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa awasili Mkoani Kagera kwa ziara ya
siku tatu kuanzia Machi 13 hadi 15, 2016
katika Manispaa ya Bukoba, Wilaya za Missenyi, Karagwe na Ngara.
Akitaja malengo ya ziara yake
mara baada ya kuwasili Mkoani Kagera alisema lengo kuu la ziara yake ni kwenda
katika ranchi za Missenyi na Kitengule
Wilayani Karagwe ili kujionea zinafanyaje kazi na kuona jinsi ya kutatua changamoto mbalimbali ili kuwepo
ufugaji bora na kuondoa migogoro ya wafugaji na wakulima.
Lengo la pili la ziara ya Mhe.
Majaliwa alisema ni kutembelea Gereza la
Mwisa Wilayani Karagwe na Ngara ili kujionea maendeleo ya wakimbizi wafungwa
wanajeshi walioletwa na Serikali katika Magereza hayo ili kuwafunza wawe raia
wema mara baada ya kubainika katika
kambi ya wakimbizi iliyopo mkoani Kigoma wakiendesha mafunzo ya kijeshi kwa
wenzao kambini.
Mara baada ya kusomewa taarifa ya
Mkoa wa Kagera na Mkuu wa Mkoa John Mongella Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
alitoa rai kwa wananchi na viongozi wa Mkoa kuhakikisha wanaulinda Mkoa ili usiingiliwe
na wahamiaji haramu kutoka nchi jirani ikiwa ni pamoja na ardhi kutouzwa
kiholela kwa wageni kutoka nje.
Aidha, Waziri Mkuu Mhe, Majaliwa
aliwaonya Wakuu wa Wilaya za Missenyi, Kyerwa na Ngara kuhakikisha wanaziba
mianya ya udhaifu ilipo kwa kuingiza mifugo na uuzwaji wa ardhi holela katika
Wilaya hizo huku wao wakiwepo kama vingozi wa Serikali, alisema wanatakiwa
kuchukua hatua haraka sana kuziba mapungufu hayo.
Pia alitoa agizo kwa Afisa
Uhamiaji wa Mkoa na Maafisa Uhamiaji wa Wilaya kuhakikisha watekeleza majukumu
yao ipasavyo na kuacha mara moja tabia ya kutoa vibali hovyo vya watu kutoka
nchi jiarani na kuhamia katika Mkoa wa Kagera na kuingiza mifugo pamoja na
kuhozi ardhi ya wazawa.
Vilevile Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa alisistiza juu ya ukusanyaji wa kodi ili Serikali iweze kuwaletea
wananchi maendeleo yao. Alihoji juu ya utoroshwaji wa Madini ya bati Wilayani
Kyerwa wakati viongozi wakiwepo bila kuchukua hatua. Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa
alisema hali hiyo inatakiwa kukoma mara moja kutorosha madini hayo kwenda nchi
jirani bila serikali kupata mapato yake.
Uzinduzin wa Miradi
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa alitembelea na
kuzindua mradi wa maji Bunena ambao ujengwa
katika Maispaa ya Bukoba kwa ufadhili wa Serikali ya Ufaransa na
umekamilika kwa asilimia 98% na gharama ya mradi huo ni zaidi ya shilingi
bilioni 31na unatarajiwa kukabidhiwa mwezi Aprili 2016 mara baada ya kuwa
umekamilika kwa asilimia mia moja.
Pia Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa alizindua kiwanda cha Maji cha Bunena Spring Water ambacho kinazalisha
maji ya kunywa na kimejengwa na Kanisa Katoliki likishirikiana na wawekezaji
wawili wazawa. Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha maji safi na salaama ya
kunywa chupa za Mililita 600 milioni tatu kwa siku.
wazawa. Kiwanda hicho kina uwezo
wa kuzalisha maji safi na salaama ya kunywa chupa za Mililita 600 milioni tatu
kwa siku.
Mkutano na Watumishi wa
Serikali
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa pia
aliongea na watumishi wa Serikali Mkoani Kagera kwa kuwa kumbusha maadili ya
kazi zao kwa kusema kuwa wajibu wa mtumishi wa Serikali ni kumpokea mwananchi,
kumsikiliza, na kumhudumia au kumwelekeza mahali pa kupata huduma stahili bila
kinyongo au kukasirika.
“Najua kuwa watumishi wa kada
mbalimbali mnaidai Serikali stahiki zenu, Serikali ya awamu ya tano imejipanga
kuhakikisha inalipa madeni ya watumishi na kwasababu hiyo nawaombeni watumishi msitumie kigezo hicho cha kuidai
serikali kufanya fujo au kukataa kuwahudumia wananchi. Alisistiza Waziri Mkuu
Mhe. Majaliwa
Mkutano wa Hadhara
Akiongea na wananchi wa Manispaa ya Bukoba katika uwanja wa Uhuru
pamoja na kero mbalimbali walizoziwasilisha kwake ikiwa mojawapo ni kero ya
wananchi waliopimiwa viwanja 800 na hawakugawiwa viwanja hivyo, Mhe. Majaliwa
alitoa muda wa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi na Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Bukoba kuwa wawe wametafuta utatuzi wa
mgogoro huo pia aliagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa fedha za serikali kuja kufanya ukaguzi
kuhusu viwanja hivyo.